Tuesday, July 31, 2012

Kuhusu mgomo wa Waalim, Serikali yahaha...

Wanafunzi wakicheza baada ya walimu wao kugoma.


WALIMU WAGOMA KILA KONA, WANAFUNZI NAO WACHACHAMAA, SERIKALI YAONYA, YATISHIA KUWAFUTIA MISHAHARA

NCHI imetikiswa. Mgomo wa walimu ulioanza jana katika sehemu mbalimbali nchini, umeathiri kwa kiasi kikubwa sekta ya elimu huku kukiwa na taarifa za matukio yasiyokuwa ya kawaida yaliyoambatana na mgomo huo usio na ukomo.

Katika sehemu mbalimbali nchini, walimu waliripotiwa kugoma kwa kutoingia madarasani na wengine walifika kazini na kusaini vitabu vya mahudhurio kisha kuondoka hali iliyosababisha wanafunzi kurandaranda ovyo katika sehemu za miji iliyo karibu na shule hizo.

Mjini Dodoma ,wabunge jana walimbana Naibu Spika, Job Ndugai wakitaka shughuli za Bunge zisitishwe ili kujadili mgomo wa walimu ambao umeanza rasmi jana nchi nzima, na kuziacha shule nyingi zikiwa na walimu wakuu na wakuu wa shule pekee.

Hata hivyo, Ndugai alisema Bunge lisingeweza kujadili suala hilo kwani tayari Serikali ilikuwa imelifikisha mahakamani baada ya kushindwa kuafikiana na walimu katika ngazi ya usuluhishi.Wakati hayo yakiendelea, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa amesema Serikali itafuta mishahara kwa walimu walioitikia mwito Chama cha Walimu Tanzania (CWT) wa kushiriki mgomo ambao alisema siyo halali.

Katika mkutano wake na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Dk Kawambwa pia aliwaonya walimu ambao alisema wamekuwa wakiwabughudhi wenzao ambao waliamua kwenda kazini.
Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo akiwa Mjini Morogoro aliwaagiza wakuu wa shule za msingi na sekondari mkoani humo kuandaa orodha ya majina ya walimu wasiofika kazini Julai 30 na waifikishe kwa maofisa elimu wa wilaya kabla ya saa 2:00 asubuhi ya Julai 31.

Waandishi wetu katika sehemu mbalimbali nchini pia waliripoti kwamba katika baadhi ya shule, wanafunzi waliruhusiwa kurejea nyumbani mapema kwa maelezo kwamba hakukuwa na masomo.Hali hiyo ilizua kizaazaa kwani katika baadhi ya mikoa wanafunzi walicharuka na kuitisha maandamano hadi katika ofisi za maofisa elimu wa wilaya, wakitaka Serikali iingilie kati mgomo huo ili waendelee kusoma.

Kadhalika, baadhi ya viongozi na watendaji wa Serikali walinukuliwa wakitoa matamko ya kuwasihi au kuwaamuru walimu warejee madarasani, kauli ambazo hata hivyo, hazikubadili uamuzi wa walimu hao.

Wanafunzi waandamana
Maandamano ya wanafunzi yaliripotiwa katika Mji wa Tunduma, Mbeya ambako polisi walitumia mabomu ya machozi kuwadhibiti wanafunzi.

Wanafunzi wa shule mbalimbali za msingi katika Wilaya ya Mbozi mkoani humo waliandamana wakidai haki ya kufundishwa. Hata hivyo, maandamano hayo yaliingiliwa na vibaka ambao baadaye walivunja ofisi za Halmashauri ya Mji wa Tunduma na kuiba mali kadhaa kisha kuchoma nyaraka zilizokuwemo.

Tukio hilo lilitokea asubuhi wakati wanafunzi wa shule 14 za msingi zilizopo katika halmashauri ya Tunduma walipojikusanya na kufanya maandamano hadi nyumbani kwa diwani na baada ya kumkosa walielekea kituo cha polisi na baadaye ofisi katika hizo.

Chanzo: http://www.mwananchi.co.tz

BAVICHA nao wanena kuhusu Mwanahalisi...


Kwa niaba ya Baraza la Vijana wa CHADEMA (BAVICHA) tukiwa ni sehemu ya wadau wa sekta ya habari nchini, tunaunga mkono maandamano ya amani mliyoitisha ya kupinga hatua ya serikali kulifungia gazeti la MwahaHALISI.

Tunawapongeza wahariri kwa mshikamano wenu katika kipindi hiki cha majaribu; endeleeni kusimama pamoja, ni umoja wenu ndio utakaokuwa kinga ya pamoja dhidi mtu au chombo chombo chochote kinachoingilia uhuru wenu. Mshikamano wenu ni ishara ya kushindwa kwa mkakati wa ‘wagawe uwatawale’ na imani kwamba umoja ni nguvu. Wahariri wote hawapaswi kukaa kimya kuhusu kufungiwa kwa MwanaHALISI kwa kuwa leo ni kwa gazeti hilo, kesho itakuwa kwa gazeti lingine; hivyo ni vyema kuungana pamoja kulinda uhuru, taaluma na sekta ya habari nchini.

Kwetu sisi hatua hiyo ya serikali tunaitafsiri zaidi ya kufungia gazeti la MwanaHALISI; ni hatua ya kufungia uhuru wa kusambaza habari na uhuru wa kupokea habari. Hivyo hatua hiyo ni kinyume cha haki za binadamu, kinyume cha utawala bora na ni kikwazo kwa demokrasia na maendeleo. Hakika serikali na viongozi wake wamevuka mstari wa kukubali kukosolewa na sasa wameamua kuanza kufungia uhuru wa fikra mbadala.

Hatua ya Waziri mwenye dhamana na sekta ya habari kugeuka mlalamikaji, mwendesha mashtaka na mfungaji ni mwelekeo mbovu wa kupuuza taasisi za kusimamia uwajibikaji na haki. Uamuzi uliofanywa na serikali hauna tofauti na unaofanywa na raia wanaojichukulia sheria mikononi(mob justice). Kwa serikali inayoheshimu misingi ya asili ya haki, tulitarajia chombo chochote cha habari, kikivunja sheria ama kukiuka maadili dhidi ya serikali, viongozi wake ama watu binafsi mashtaka ama malalamiko yangepelekwa kwa taasisi zinazohusika mathalani Baraza la Habari(MCT) ama Mahakama.

Hatua ya serikali kufungia gazeti la MwanaHALISI pamoja na kuwa imechukuliwa kwa mujibu wa sheria iliyopo, imekiuka misingi ya asili ya utawala wa sheria. Kwani kulikuwa na sheria nyingine nzuri ambazo serikali ingeweza kutumia kupitia mahakama lakini ikaamua kuchagua kutumia sheria mbaya kwa kutumia mamlaka ya Waziri. Itakumbukwa kwamba wadau wa sekta ya habari na hata serikali yenyewe imekuwa ikikiri kwamba Sheria hiyo iliyotumiwa ni sheria mbovu inayohitaji kufutwa ama kufanyiwa marekebisho makubwa ikiwemo kupunguza mamlaka makubwa ya viongozi wa serikali dhidi ya vyombo vya habari. Sheria yoyote inayotambulika kuwa mbovu katika jamii yoyote, inapoteza uhalali wa kihaki(legitimacy) miongoni mwa umma na hivyo kuendelea kuitumia ni kuteteresha misingi ya utawala wa sheria na kutoa mfano mbaya kwa vijana nchini na wananchi kwa ujumla. Hivyo, tunachukua fursa hii kuitaka serikali kuharakisha mchakato wa kupitisha sheria ya vyombo habari na sheria ya uhuru wa taarifa.

Aidha tumeshangazwa na uamuzi wa serikali kufanya maamuzi yake kwa ubaguzi kwa kulichukulia hatua gazeti la MwanaHALISI na kukwepa kuyachukulia hatua magazeti mengine ambayo yameandika habari inayoshabihiana na maudhui ya habari iliyoandikwa na gazeti hilo. Kwa muda mrefu sasa, habari za uwepo wa viongozi ama makundi ndani ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) yenye kupanga ‘kumng’oa’ Rais Jakaya Kikwete miongoni mwa wanaotarajiwa kugombea urais kupitia chama hicho mwaka 2010 zimeandikwa na magazeti mbalimbali. Hatua hii ya kibaguzi inaibua maswali kuhusu dhamira ya serikali kulifungia gazeti hilo wakati huu ambapo mchango wa gazeti hilo na mengine yaliyo mstari wa mbele kupinga ufisadi na kutetea rasilimali za taifa unahitajika kwa kiasi kikubwa. Hata baada ya kulifungia gazeti la MwanaHALISI, habari za aina hiyo zimeendelea kuandikwa ikiwemo na vyombo vya habari vya nje; mathalani tarehe 24 Oktoba, 2008 kutoka Ufaransa gazeti la Africa Intelligence inayomtaja Rostam Aziz kukusanya fedha kwa ajili ya kufadhili kundi lake katika uchaguzi huo. Katika muktadha huo, serikali inapaswa kulifungia gazeti la MwanaHALISI mara moja, kama imeonyesha wazi kushindwa kuyachukulia hatua magazeti mengine.

Kadhalika kwa mtiririko wa matukio katika taifa letu, kuna mwelekeo wa Serikali na CCM kuminya maoni yenye kumkosoa au kumgusa Rais Kikwete. Mjadala wa Rais Kikwete ‘kung’olewa’ katika uchaguzi mwaka 2010 unaelekea kuichukiza kwa kiasi kikubwa Serikali na CCM. Gazeti la MwanaHALISI liliandika habari ya namna hiyo, likafungiwa na Serikali. Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe akiwa katika ‘Operesheni Sangara’, alitoa hoja hiyo na matokeo yake CCM ikaibuka na kujibu kwa vitisho na vioja.

 Vijana wa Tanzania wangependa kupata mfano uongozi bora wenye kukubali kukosolewa na kukubali mabadiliko badala ya uongozi legelege wenye kuendeleza udikitekta wa kimawazo na hivyo kuminya fikra huru. Si dhambi kwa CHADEMA ama mtu yoyote kutaka kuiondoa CCM ama kiongozi wake yoyote madarakani mwaka 2010 kupitia njia za kidemokrasia.

Mwisho, tunatoa mwito kwa watanzania wote kusoma alama za nyakati na kuunga mkono harakati hizi za wahariri na wadau wa sekta ya habari kutetea uhuru wa kweli katika taifa letu. Jamii itambue kwamba kitisho cha uhuru na haki kwa mtu Fulani au mahali Fulani ni tishio kwa watu wote na mahali pote. Yanayofanywa kwa vyombo vya habari, yanaweza pia kufanywa kwa watetezi wengine kwani hivi karibuni taifa limeshuhudia Asasi ya HAKIELIMU ikitishiwa kutokana na jitihada zake za kuhamasisha mabadiliko ya fikra katika sekta ya elimu na kupiga vita ufisadi unaoathiri sekta hiyo. Tuko katika kipindi cha majaribu; kuibuka kwa mijadala yenye kuchochea mgawanyiko/ubaguzi, kuongezeka kwa matabaka na malalamiko juu ya hali za maisha. Katika wakati huu ambapo misingi ya nchi yetu iliyopo katika Ngao ya Taifa ya Uhuru na Umoja inapotikiswa ni wakati wa kuunganisha “Nguvu ya Umma” kupinga aina zote za ufisadi na kutetea rasilimali za taifa kwa kuhamasisha maadili, fikra mbadala na mabadiliko ya kweli. Kuunga mkono maandamano ya wadau wa sekta ya habari ni sehemu ya azma hiyo. Mshikamano, daima; pamoja, tutashinda!

Wasalaam,

John Mnyika
Mkurugenzi wa Vijana Taifa.

TAMKO LA CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA)




KUHUSU KUFUNGIWA KWA MWANAHALISI

Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kinalaani uamuzi wa Serikali inayoongozwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kulifungia kwa muda usiojulikana gazeti la MwanaHalisi kwa kutumia mwanya wa sheria mbovu ya magazeti inayokwenda kinyume na haki za binadamu na utawala bora.

CHADEMA kinaitaka Serikali kulifungulia gazeti hilo haraka iwekanavyo na kimewasiliana na Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inayoongozwa na CHADEMA kuchukua hatua za kibunge kuisimamia Serikali kurekebisha udhaifu huo ikiwa inaheshimu uhuru wa habari na inazingatia maslahi ya taifa.

CHADEMA kinatafsiri hatua hiyo ya Serikali ya kufungia gazeti la MwanaHalisi kuwa ni sawa na kufungia uhuru wa kusambaza habari, uhuru wa kupokea habari na uhuru wa kutoa maoni, hivyo tunatoa mwito kwa wananchi na wadau wote wa habari kuungana pamoja kupinga hatua hiyo, na CHADEMA kitaeleza hatua za ziada za kuchukuliwa iwapo Serikali haitasikiliza kauli za wadau wa habari juu ya suala hili.

CHADEMA kinatambua kuwa uamuzi wa Serikali kufungia gazeti hilo kwa mara nyingine tena ni kwenda kinyume na haki za binadamu, kinyume na utawala bora na ni kikwazo kwa demokrasia na maendeleo nchini.

CHADEMA kinapinga hatua ya Serikali ambayo viongozi na watendaji wake wakiwa wametajwa kama watuhumiwa katika habari zilizoandikwa na gazeti hilo imetumia mamlaka haramu ya Waziri mwenye dhamana ya sekta ya habari kugeuka mlalamikaji, mwendesha mashtaka na mfungaji huku ikipuuza taasisi za kusimamia uwajibikaji na haki.

CHADEMA ilitarajia badala ya kulifungia gazeti la MwanaHalisi ingewezesha kufanyika kwa uchunguzi huru kufuatia habari za kiuchunguzi zilizoandikwa na gazeti hilo juu ya watendaji na watumishi wa Serikali kuhusishwa na jaribio la mauji ya Dr Ulimboka Steven, kupanga njama za mauji ya viongozi wa CHADEMA na matukio mengine ambayo yenyewe ndiyo yenye mwelekeo wa kufanya wananchi wapoteze imani na vyombo vya dola hali ambayo inaweza kuhatarisha amani na mshikamano uliopo nchini.

CHADEMA kinalinganisha uamuzi huo wa Serikali uliotangazwa tarehe 30 Julai 2012 na Msajili wa Magazeti chini ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kuwa ni sawa kujichukulia sheria mikononi kwa kuwa Serikali yenye kuheshimu misingi ya asili ya haki ingezingatia kwamba ikiwa chombo chochote cha habari kimedaiwa kuvunja sheria ama kukiuka maadili dhidi ya Serikali, viongozi wake ama watu binafsi mashtaka au malalamiko yangepelekwa kwa taasisi zinazohusika mathalani Baraza la Habari (MCT) au mahakama.

CHADEMA kinafahamu kuwa Serikali imeamua kulifungia kutochapishwa kwa muda usiojulikana gazeti la MwanaHalisi, kwa mujibu wa Sheria ya Magazeti ya mwaka 1976, kifungu Na. (25) (i); hata hivyo uamuzi huo ni kinyume cha misingi ya asili ya utawala wa sheria.

CHADEMA kinaelewa kwamba zipo sheria nyingine katika nchi yetu ambazo Serikali ingeweza kuzitumia kushughulikia madai iliyoyatoa kuwa Gazeti la Mwanahalisi limeandika habari na makala za uchochezi, uhasama na uzushi kupitia mahakama lakini imeamua kwa makusudi kuendelea kutumia sheria mbaya isiyokuwa na uhalali wa kihaki (illegitimate).

CHADEMA kinakumbusha kuwa kwamba Sheria hiyo ni kati ya Sheria zilizotajwa na Tume ya kukusanya maoni juu ya mfumo wa vyama vingi (Tume ya Nyalali) kuwa ni sheria mbaya miaka 20 iliyopita kuwa na Sheria mbaya na Serikali imekuwa ikikwepa kutunga sheria mpya pamoja na wadau wa habari kuandaa miswada ya sheria ya huduma za vyombo vya habari na uhuru wa taarifa kwa nyakati mbalimbali.

CHADEMA kinatoa mwito kwa wananchi na taasisi zote za kitaifa na kimataifa kufuatilia kwa karibu tukio hili la kufungiwa kwa gazeti la MwanaHalisi na matukio mengine ya hivi karibuni kuhusu asasi za kiraia, makundi mbalimbali katika jamii ikiwemo madaktari na vyama vya siasa hususan CHADEMA yenye kuashiria kwamba Serikali inayoongozwa na CCM imeanza mkakati wa kuficha ukweli na kudhibiti mabadiliko kwa kutumia sheria kandamizi, vyombo vya dola na njia nyingine haramu.

Hivyo, ieleweke kwamba hatua hii dhidi ya Gazeti la MwanaHalisi ni mwanzo tu wa hatua zingine zaidi dhidi ya magazeti mengine na taasisi nyingine hali ambayo inahitaji wananchi na wadau wote kuunganisha nguvu za pamoja katika kuchukua hatua za haraka kuinusuru nchi na mwelekeo huo.

Imetolewa tarehe 30 Julai 2012 na:

John Mnyika (Mb)
Mkurugenzi wa Habari na Uenezi

Wakati walimu wanagoma Wabunge wanaongezewa 'mihela'


MARUPURUPU ya wabunge ikiwamo mishahara imeongezwa kutoka Sh7.4 milioni kwa mwezi hadi takriban Sh11milioni kwa mwezi, hatua ambayo imeibua mjadala mwingine mzito miongoni mwao.

Tangu mwaka jana, wabunge wamekuwa katika vita ya kupokea au kutopokea posho ya vikao ambayo imekuwa ikikolezwa na Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe ambaye alizikataa akisema mbunge anapokuwa kazini hahitaji kulipwa.

Hata hivyo, uchunguzi wa gazeti hili umebaini kwamba sasa vita kubwa ipo katika marupurupu mapya ambayo pamoja na kuchanganya na mshahara yanafikia Sh11milioni kwa mwezi.

Spika wa Bunge, Anne Makinda alipoulizwa jana alithibitisha kuhusu kuongezeka kwa malipo jumla ya wabunge kwa mwezi lakini akasema hafahamu kiwango halisi kilichoongezwa.

Makinda alisema nyongeza iliyopo siyo kwa wabunge tu, bali watumishi wote wa Serikali na ilitangazwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma), wakati wa Bajeti ya Ofisi hiyo kwa mwaka 2012/13.

“Hiyo nyongeza siyo tu kwa wabunge, bali ni kwa watumishi wa Serikali. Tena hiyo ilitangazwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma). Sasa ukiniuliza kiasi gani hapo ndipo sielewei, ila najua nyongeza ipo,” alisema Spika.

Lakini, vyanzo kutoka ndani ya Bunge vilisema kwamba nyongeza hiyo ambayo tayari imeingia katika mshahara wa Julai ni Sh3.6milioni, hivyo kufanya jumla ya fedha anazochukua mbunge kufikia kiasi hicho cha Sh11milioni.
“Hiyo ni vita, kuna wabunge wana hasira kweli hawataki wananchi wajue kama marupurupu yameongezeka.

Wanaona wananchi wakijua itakuwa ni tatizo kubwa, watapigiwa kelele lakini nyongeza hiyo ipo. Tayari wengine wamechukua tangu Ijumaa,” kilisema chanzo kimoja kwa sharti la kutotajwa jina gazetini.

Hata hivyo, kwa mujibu wa chanzo hicho, baadhi ya wabunge kutoka kundi la wanaopinga posho kwa wabunge wamepinga pia nyongeza hiyo wakitaka fedha hizo zielekezwe katika sekta nyingine za kijamii.

Marupuru ya sasa
Hadi mwezi uliopita, mbunge alikuwa akipokea Sh7.4milioni kwa mwezi ambazo kati ya hizo Sh2.5milioni ni kwa ajili ya mafuta, Sh2.3 mshahara, Sh170,000 kwa ajili ya mshahara wa dereva, 100,000 kwa ajili ya katibu wa mbunge na posho ya jimbo.

Hata hivyo, katika nyongeza hiyo ya sasa haijawekwa wazi kwamba kiasi gani ni kwa ajili ya mshahara, fedha za mafuta ya gari la mbunge, za dereva, katibu na za posho ya jimbo na tayari baadhi ya wabunge wameanza kufuatilia mchanganuo wa nyongeza hiyo.

Chanzo:

Futari ya leo,

Asalam Alaykum,

Leo tutapika futari ya kipwani, Mihogo ya nazi, maharage ya sukari, chapati na mchuzi wa kukaanga, papa wa kuchoma na nyama ya kuchemsha iliyokaushwa na viungo kama pilipili manga, tangawizi, limao na vitunguu swaum.

Halafu unamalizia na matunda kama kawaida yetu, ukipata aina mbili za matunda itakuwa vema. Maji mengi ni muhimu usisahau.

Mhhhh Hapo siongezi neno wadau....


Biashara haramu yashamiri katika jeshi la Guinea Bissau..



Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeonyesha wasiwasi wake juu ya kuongezeka kwa biashara ya dawa za kulevya Guinea-Bissau tangu mapinduzi yatokee mwezi April.
Limetaka viongozi nchini humo kurejesha utawaa wa kikatiba.
Guinea-Bissau imekuwa na hisotria ya mapinduzi tangu uhuru wake kutoka kwa Mreno mwaka 1974.
Imekuwa ndio kitovu cha magenge ya kupitishia cocaine kutoka Latin America mpaka Ulaya, ikituhumiwa kushirikiana na maafisa wa jeshi.
"Wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wamelaani kitendo cha jeshi kuingilia siasa na kuonyesha wasiwasi wake kuhusu taarifa za kuongezeka kwa usafirishaji wa dawa kuongezeka tangu April 12 mapinduzi yalipotokea." Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilisema katika mkutano wake New York.
Limesema lilikuwa linaangalia uwezekano wa mkutano wa kimataifa kuzungumzia ni kwa namna gani watafanikiwa kurejesha utawala wa kidemokrasia nchini Guinea Bissau.
'Ushawishi'
Mwezi Mei , Baraza hilo liliweka vikwazo vya kusafiri kwa viongozi wa mapinduzi na wanaowaunga mkono.
Jeshi limekubali mazungumzo yasimamiwe na ECOWAS, kurejesha nchi katika utawala wa demokrasia lakini limeshindwa kufanya hivyo.
Mwaka 2010, Marekani iliwashutumu wanajeshi kutoka Guinea-Bissau, wakiwemo mkuu wa jeshi la majini Jose Americo Bubo Na Tchuto, kwa kuhusika na dawa za kulevya.
Katika sheria ya Ushawishi wa Dawa za kulevya , vikwazo vya kifedha viliwekwa.
Hakuna wa kuchaguliwa kwa karibu miaka arobaini sasa ya uhuru ambaye amewahi kumaliza muda wake wa uongozi nchini Guinea-Bissau.
Chanzo: BBC Swahili

Raia wa Marekani akiri kuisaidia Al shabab....


Mmarekani aliyetuhumiwa kwa kujaribu kujiunga na kundi lenye msimamo mkali la Kiislam la al-Shabab nchini Somalia amekiri mashtaka yake kwenye mahakama Marekani.
Shaker Masri, 28, alikamatwa Agosti 2010 akijiandaa kusafiri kwenda Somalia kukijunga na al-Shabab, kwa mujibu wa mwendesha mashtaka wa Marekani.
Marekani na Uingereza wanaliona kundi hilo likijihusisha na al-Qaeda, kuwa ni kundi la kigaidi.
Katika makubaliano ya kukubali mashtaka, Masri amekubali kutumikia kifungo chini ya miaka kumi gerezani.
Alikiri kupanga njama za kukusanya fedha alizohitaji kujzitumia katika jihadi ama Somalia au Afghanistan.
Amehukumiwa kifungo za miaka 15 gerezani.
Masri alizaliwa Alabama na kuishi Chicago kabla ya kukamatwa saa chache hajaondoka nchini.
Amekuwa akijieleza kama wakala wa FBI wa siri na amekuwa akizungumzia kuhusu kuwalenga ‘makafiri’
Kufuatia kukamatwa kwake alishtakiwa kwa kujaribu kusaidia kwa mali kundi la kigaidi, akijaribu kuwapa msaada kwa kutumia silaha za maangamizi.
Taarifa kamili za kukiri kwake hazijatolewa kwa umma.
Al-Shabab wanaamini kuwa ikiwapata wasomali wenye asili ya Kimarekani kushiriki katika kujitoa muhanga nchini Somalia na maafisa wa Marekani sasa wana wasiwasi wa kuwepo shambulio ndani ya Marekani.
Raia kadhaa wa Marekani wamekamatwa katika miaka ya karibuni wakijaribu kushiriki au kuunga mkono vita vya zaidi ya miongo miwili iliyopita.
Shaker Masri atahukumiwa rasmi mwezi Oktoba 16.
Chanzo: BBC Swahili.

CCM yamjia juu Tundu Lissu.


Na Hafidh Kido

Katibu wa itikadi na uenezi chama cha mapinduzi (CCM) Nape Nnauye, amemtaka mnadhimu mkuu wa kambi ya upinzani bungeni na mbunge wa Singida Mashariki (chadema) Tundu Lissu, kuacha kuingilia shughuli za kamati zilizoundwa kufuatilia suala la wabunge wanaohusishwa na rushwa kutoka shirika la umeme nchini TANESCO.

Akizungumza jijini Dar es Salaam leo asubuhi Nape alisema anasikitishwa na kitendo cha Lissu, kutaja majina ya wabunge wanaotuhumiwa kwa rushwa katika sakata hilo lakini cha kusikitisha ametaja majina mengi ya wabunge wa CCM wakati wapo wabunge wa vyama vya upinzani ambapo watanzania wanawatajataja kila siku.

“Si kitendo cha kizalendo hata kidogo kuanza kutaja wabunge wanaohusishwa na rushwa hii, tena cha kusikitisha wabunge wengi wametajwa kutoka chama changu. Wapo wabunge kutoka upinzani ambao wanatajwa tena wengi ni wa chadema, mbona sisi hatuwataji,” alihoji Nape.

Aidha katibu huyo wa itikadi na uenezi alifafanua kuwa ni vema kazi hiyo wakaachiwa kamati zilizopangwa na kama wapo watu aina ya kina Tundu Lissu, ambao wanazo taarifa za kutosha waende kuzisaidia kamati hizo ili kupatikana watuhumiwa hawa maana sisi tunalaani vitendo vya rushwa.

“Wakati ukifika kina Lissu wataitwa kutoa ushahidi, lakini kwa sasa tunalaani kila anaetaka kuhujumu shughuli hii ya kuwahoji watuhumiwa wa rushwa. Maana rushwa inayomgusa kiongozi wa umma hiyo inakuwa zaidi ya rushwa, ni hujuma dhidi ya uchumi wetu,” alisisitiza.

Wakati akijibu maswali ya waandisi wa habari Nape alieleza kuwa iwapo wabunge wa CCM watakutwa na hatia chama kitawafutia uanachama maana huo ndiwo utaratibu wa chama chao kawaida hakilindi wala rushwa.

“Unajua watu wanadhani sisi tunakumbatia wala rushwa, nataka kuwahakikishia kuwa CCM ndiyo chama kinachoongoza kutimua wanachama wake walihusishwa na rushwa. Nawaahidi iwapo mbunge wa chama changu atabainika kuhusika kufanya biashara na TANESCO ama kula rushwa kinyume na taratibu tutamfutia uanachama maana hiyo ipo wazi hata katika kanuni zetu tunatamka kuwa ‘rushwa ni adui wa haki sipokei wala sitoi rushwa,” alieleza.

Suala hili la shirika la umeme nchini TANESCO na wabunge lilianza wiki chache zilizopita baada ya mkurugenzi wa shirika William Mhando, hilo kusimamishwa Katibu mkuu wa wizara ya nishati na madini EliakimMaswi ili kupisha uchunguzi wa shutuma za kutumia vibaya madaraka yake katika shirika hilo.

Hata hivyo baadhi ya wabunge akiwemo mbunge wa Kigoma kusini Zitto Kabwe (chadema) walilaani hatua hiyo ya kusimamishwa  kwa William Mhando na kuanza kuibua masuala mengine kama kupatikana zabuni ya kuiuzia TANESCO mafuta ya kuendeshea mitambo ya kuzalisha umeme kutoka kampuni ya mafuta ya PUMA energy. Na ndipo pakazuka madai kuwa hata baadhi ya wabune wapo ambao walihusika kufanya biashara na shirika hilo la umeme nchini ambapo walihusishwa na rushwa.

HAFIDH KIDO
DAR ES SALAAM, TANZANIA
31/07/2012

Wanawake wa Kiafrika ni wazuri... ati.




I just adored this photo with the caption....


Hebu nisaidie kutafsiri picha hii, huyu jamaa anajaribu kumwambia nini huyu binti?


TFF Taarifa kwa vyombo vya habari


Release No. 128



TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Julai 31, 2012

MECHI YA NGORONGORO HEROES YAINGIZA MIL 12/-
Mechi ya kwanza ya raundi ya pili kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Afrika kwa vijana chini ya umri wa miaka 20 kati ya Tanzania (Ngorongoro Heroes) na Nigeria (Flying Eagles) iliyochezwa juzi (Julai 29 mwaka huu) imeingiza sh. 12,901,000.

Fedha hizo zimepatikana kutokana na watazamaji 3,377 waliokata tiketi kushuhudia pambano hilo lililochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Sehemu iliyoingiza watazamaji wengi ilikuwa viti vya bluu na kijani ambapo 2,697 walikata tiketi kwa kiingilio cha sh. 3,000 kila mmoja. Viingilio vingine katika mechi hiyo vilikuwa sh. 5,000 kwa viti vya rangi ya chungwa, sh. 10,000 kwa VIP C na B, na sh. 15,000 kwa VIP A iliyoingiza watazamaji 21.

Mgawanyo wa mapato hayo ni kama ifuatavyo; asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) ilikuwa sh. 1,967,949.15, gharama ya kuchapa tiketi sh. 2,250,000, gharama za waamuzi na kamishna wa mechi hiyo sh. 760,000 na ulinzi na usafi kwa Uwanja wa Taifa sh. 2,350,000.

Malipo kwa Wachina (Beijing Construction) sh. 2,000,000, asilimia 20 ya gharama za mchezo ni sh. 714,610.17, asilimia 10 ya uwanja sh. 357,305.08, asilimia 5 ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) sh. 178,652.54 na asilimia 65 ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) sh. 2,322,483.05.

Mechi ya marudiano ya michuano hiyo ambayo fainali zake zitafanyika mwakani nchini Algeria itachezwa Agosti 12 mwaka mjini Ilorin, Jimbo la Kwara, Nigeria.



PONGEZI KWA UONGOZI MPYA SIREFA
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linatoa pongezi kwa uongozi mpya wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Singida (DOREFA) uliochaguliwa katika uchaguzi uliofanyika Julai 28 mwaka huu.

Ushindi waliopata viongozi waliochaguliwa kuongoza chama hicho unaonesha jinsi wajumbe wa Mkutano Mkuu wa SIREFA walivyo na imani kubwa kwao katika kusimamia mchezo huo mkoani Singida.

TFF inaahidi kuendeleza ushirikiano wake kwa Kamati ya Utendaji ya SIREFA chini ya uenyekiti wa Baltazar Kimario ambaye amechaguliwa kwa mara ya kwanza.

Uongozi huo mpya una changamoto nyingi, kubwa ikiwa ni kuhakikisha unaendesha shughuli za mpira wa miguu mkoani Singida kwa kuzingatia katiba ya SIREFA pamoja na vyombo vya mpira wa miguu vilivyo juu yake.

Pia tunatoa pongezi kwa Kamati ya Uchaguzi ya SIREFA na Kamati ya Uchaguzi ya TFF kwa kuhakikisha uchaguzi huo unaendeshwa kwa mujibu wa kanuni za uchaguzi za wanachama wa TFF.

Viongozi waliochaguliwa katika uchaguzi huo uliofanyika Chuo Cha Maendeleo ya Jamii Singida ni Baltazar Kimario (Mwenyekiti), Hussein Mwamba (Katibu Mkuu), Gabriel Gunda (Katibu Msaidizi), Gabriel Mwanga (Mhazini), Hamisi Kitila (Mjumbe wa Mkutano Mkuu TFF), Omari Salum (Mwakilishi wa Klabu TFF), Yagi Kiaratu na Dafi Dafi (wajumbe wa Kamati ya Utendaji).

Nafasi za Makamu Mwenyekiti, Mhazini Msaidizi na wajumbe wawili wa Kamati ya Utendaji zitajazwa katika uchaguzi mdogo utakaofanyika baadaye.



MICHELSEN AITA 22 KAMBI YA COCA-COLA
Kocha wa timu za Taifa za vijana za Tanzania, Jakob Michelsen ameita wachezaji 22 kwa ajili ya michuano ya kimataifa ya Coca-Cola itakayofanyika baadaye mwaka huu nchini Afrika Kusini.

Baadaye watachujwa na kubaki 16 ambao ndiyo watakaokwenda kwenye michuano ya Afrika Kusini. Wachezaji waliochaguliwa wametokana na michuano ya Copa Coca-Cola iliyofanyika jijini Dar es Salaam na mkoani Pwani kuanzia Juni 24- Julai 2 mwaka huu.

Wachezaji walioitwa ni Abdulrahman Mandawanga (Dodoma), Abraham Mohamed (Mjini Magharibi), Ayoub Alfan (Dodoma), Bakari Masoud (Tanga), Daniel Justin (Dodoma), Denis Dionis (Ilala), Edward Songo (Ruvuma), Fikiri Bakari (Tanga), Hassan Kabunda (Temeke), Joseph Chidyalo (Dodoma), Mutalemwa Katunzi (Morogoro) na Mwarami Maundu (Lindi).

Wengine ni Nankoveka Mohamed (Ilala), Nelson Peter (Morogoro), Omari Saleh (Singida), Rajab Rajab (Mwanza), Said Said (Kagera), Shiza Kichuya (Morogoro), Shukuru Msuvi (Temeke), Tanganyika Suleiman (Kigoma), Tumaini Baraka (Kilimanjaro) na William John (Ruvuma).

Pia Michelsen ameongeza wachezaji saba kwenye kikosi cha Serengeti Boys ambacho Septemba mwaka huu kitacheza na Kenya kuwania tiketi ya fainali za vijana wenye umri chini ya miaka 17 za Afrika zitakazofanyika mwakani nchini Morocco.

Wachezaji walioongezwa kwenye kikosi hicho ambao pia wametoka kwenye Copa Coca-Cola ni Abdallah Baker (Mjini Magharibi), Abdallah Kheri (Mjini Magharibi), Calvin Manyika (Rukwa), Dickson Ambunda (Mwanza), Hassan Mganga (Morogoro), Miza Abdallah (Kinondoni) na Mzamiru Said (Morogoro).



Boniface Wambura

Ofisa Habari

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

UVCCM yatangaza ufunguzi wa kuchukua fomu za kugombea..


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI



MCHAKATO WA UCHAGUZI MKUU WA UVCCM TAIFA

                             

UMOJA WA VIJANA WA CHAMA CHA MAPINDUZI UNAWATANGAZIA WANACHAMA WAKE WENYE SIFA ZA KUGOMBEA NAFASI ZA UONGOZI WAJITOKEZE KUCHUKUA NA KURUDISHA FOMU.

MUDA WA KUCHUKUA NA KURUDISHA FOMU ZA KUGOMBEA KWA NAFASI ZOTE NGAZI YA MKOA NA TAIFA NI KUANZIA TAREHE 1/08/2012 SAA 2.00 ASUBUHI HADI TAREHE 6/08/2012 SAA 10.00 JIONI.



NGAZI YA TAIFA NAFASI ZITAKAZOGOMBEWA NI:-

(i)                  MWENYEKITI WA UVCCM TAIFA



(ii)                 MAKAMU MWENYEKITI WA UVCCM TAIFA



                

(iii)                WAJUMBE WA HALMASHAURI KUU YA CCM TAIFA, (NAFASI SITA (6) TANZANIA BARA NA NAFASI NNE (4) TANZANIA VISIWANI)

              

(iv)               WAJUMBE WA BARAZA KUU LA UVCCM TAIFA (NAFASI TANO (5) TANZANIA BARA NA NAFASI TANO (5) TANZANIA VISIWANI)



(v)                MJUMBE MMOJA MMOJA WA KUIWAKILISHA UVCCM KATIKA VIKAO VYA JUMUIYA ZA UWT NA WAZAZI.



MWOMBAJI WA NAFASI ZILIZOTAJWA HAPO JUU ANARUHUSIWA KUCHUKUA NA KUREJESHA FOMU KATIKA OFISI ZA UVCCM MKOA, AFISI KUU ZANZIBAR NA MAKAO MAKUU YA UVCCM TAIFA.

KWA NAFASI YA MWENYEKITI WA UVCCM TAIFA NA MAKAMU MWENYEKITI WA UVCCM TAIFA WATATAKIWA KUREJESHA FOMU HIZO KWA KATIBU MKUU WA UVCCM TAIFA -  MAKAO MAKUU DAR ES SALAAM.

GHARAMA YA KILA FOMU KWA NAFASI ZOTE NI TSHS. 10,000/=.

HIVYO MWOMBAJI WA NAFASI ZA UONGOZI ZA UVCCM ANATAKIWA KUWA NA SIFA ZIFUATAZO:-

(i)                  AWE MWANACHAMA HAI WA UVCCM NA CCM NA ANAYETIMIZA HAKI, WAJIBU NA MASHARTI YA UANACHAMA



(ii)                 AWE NA UMRI WA KUANZIA MIAKA 18 NA ASIZIDI MIAKA 30



(iii)                AWE RAIA WA TANZANIA



AIDHA UCHAGUZI MKUU NGAZI YA WILAYA UMESOGEZWA MBELE ILI KUPISHA SIKUKUU YA EID EL FITRI NA SENSA NA SASA UTAFANYIKA KATI YA TAREHE 28/08/2012 -30/08/2012.

WANACHAMA WOTE WENYE SIFA WANAKARIBISHWA KUJITOKEZA KUGOMBEA NAFASI HIZO HAPO JUU.



KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI

IMETOLEWA NA:



MARTINE R. SHIGELA (MNEC)

KATIBU MKUU


Tanga nao hawautaki ati....... Muungano.


Burhani Yakub, Tanga
MUUNDO wa  sasa wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,unapaswa kufanyiwa marekebisho kupitia Katiba Mpya, ili kupunguza manung’uniko na hatimaye mwafaka kuhusu Muungano.
Hayo yalisemwa juzi na wananchi wa Jiji la Tanga, walipokuwa wakitoa maoni yao kwa Tume ya Kukusanya Maoni ya Wananchi kuhusu Mabadiliko ya Katiba Mpya.

Wananchi hao, wamedai kuwa muundo wa sasa wa Muungano hauna tofauti na kuwaunganisha tembo na sungura, jambo ambalo haliletin usawa.


Akitoa mapendekezo yake, Jonathan Bahweje alisema kimsingi muundo wa sasa wa chombo hichon haufai kwa sababu hakuna fursa  sawa kati ya Zanzibar na Tanzania bara.

“Muungano wa sasa ni kama tembo na sungura, unawaweka pamoja halafu unasema umewaunganisha na wako sawa, wakati kwa uhalisia, haiwezekani,” alisema Bahweja.

Mwananchi huyo alipendekeza Katiba Mpya, ivunje muungano ili usiwepo
hatimaye Tanzania bara na Zanzibar, kila moja ijitegemee na kwamba hakuna sababu ya kuogopa kuuvunja chombo hicho.

“Mimi napendekeza Muungano uvunjwe ili kila nchi iwe na Serikali yake, kwa sababu manung’uniko ni mengi na  yanayotokana na jinsi muundo wa sasa usivyokubalika,”alisema Bahweja.

Alisema kama kuna ugumu wa kuvunja Muungano, basi ni vema kukawa na  Serikali tatu, ili kila nchi iweze kuwa na uhuru wa kuendesha mambo yake wakati kuna Serikali ya Muungano itakayosimamiwa masuala yanayohusu Muungano tu.

Kwa upande wake, Rashid Juma, ambaye ni mkazi wa Kijiji cha Kivumbitifu, katika Kata ya Pongwe, alitaka Muungano uvunjwe kwa madai kuwa wananchi wa Tanzania bara wanapokwenda Zanzibar na kurejea na bidhaa, wanatozwa ushuru wakati wakiwa ndani ya nchi moja.

“Huu Muungano hauna faida kwetu wananchi wa Tanzania bara,  unasemaje wamba tumeungana lakini sisi tukienda Zanzibar tukija na bidhaa tunatozwa ushuru lakini ukipeleka kutoka bara hakuna ushuru,”alihoji Jumaa.
 Chanzo:Mwananchi


Breaaaaking News Zenawi is no more...


In shocking news for the whole of Africa, Meles Zenawi has passed away from acute justifribilasis fatilosis at the age of 57.  No other leader in the history of the theird world has done more to lift his country from the clutches of poverty and delivered Ethiopia into the forefront of modernity in less than 22 years of rule. 
His Excellency Zenawi leaves behind a country that is flourishing and his legacy will forever be etched in all Africans as an intellectual giant who has done more for Africa than Nelson Mandela could have done in five lifetimes.  Today is a sad day for all Africans as a son of Ethiopia has been called home by his maker.

Monday, July 30, 2012

Zitto Kabwe upepo wabadilika, ahojiwa kwa rushwa.


SAKATA la wabunge kuhusishwa na rushwa limeingia sura mpya, baada ya Naibu Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Zitto Kabwe kuhojiwa na chama chake cha Chadema kwa saa tatu jana.
Wakati Zitto akihojiwa, kambi rasmi ya upinzani bungeni, iliwataja wabunge saba wa CCM na kueleza kuwa ndiyo wanaolichafua Bunge kwa kujihusisha na mambo yenye maslahi binafsi wakiwa watumishi wa umma.

Kadhalika, Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai alisema kwamba Taasisi ya Kuzuia na Kupamba na Rushwa (Takukuru) ilikuwa ikiendelea kuwahoji baadhi ya wabunge kuhusu tuhuma za rushwa na kwamba uchunguzi ukikamilika taarifa zitawekwa wazi.

Zitto ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC) na Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, jana aliandika katika ukurasa wake wa mtandao wa Tweeter kwamba alihojiwa na Sekretarieti ya chama chake kutokana na tuhuma za rushwa zinazowagusa badhi ya wabunge.
Katika maelezo yake, Zitto alisema aliiambia sekretarieti ya chama hicho kwamba Chadema kifanye uchunguzi ili kubaini ukweli wa suala hilo na kwamba yuko tayari kuwajibika ikiwa itathibitika kwamba alihusika kula rushwa.

“Kwa saa tatu nimejieleza mbele ya sekretariati ya chama kuhusu tuhuma za rushwa dhidi yangu. Niliomba kutaka kutoa maelezo kwa Katibu Mkuu, nimekiomba chama kufanya uchunguzi na ikibainika hatua zichukuliwe,” inasomeka sehemu ya taarifa hiyo kwenye Tweeter.

Lissu ataja wengine
Kwa upande wake, Mnadhimu Mkuu wa kambi hiyo, Tundu Lissu aliwataja wabunge wa CCM ambao wanatuhumiwa kuwa ni Nasir Abdallah (Korogwe Mjini), Mariam Kisangi (Viti Maalumu), Vicky Kamata (Viti Maalumu) na Charles Mwijage (Muleba Kaskazini) ambao hata hivyo, wote wamekanusha madai hayo.