Mahakama nchini Namibia imetoa uamuzi wake kuwa wanawake watatu
wanaoishi na virusi vya HIV haki zao za kibinadamu zilikiukwa walipofungiwa
uzazi bila ridhaa yao .
Wanawake hao wanasema
waliambiwa wafanyiwe utaratibu huo kama
walikuwa wanataka kujifungua kwa upasuaji kupunguza uwezekano wa watoto wao
kuambukizwa virusi vya HIV.
Mahakama hiyo iaangalia ni kwa namna gani
watapata fidia ya athari walioipata. Mwandishi wa BBC Kusini mwa Afrika anasema
uamuzi huo wa mahakama kuwapa haki wanawake hao unaweza kuwa na athari chanya
kwa nchini nyingine katika ukanda huo.
Kesi
hiyo ilifunguliwa na wanawake wajawazito watatu walioamua kujifungua kwa
upasuaji ili kupunguza uwezekano wa watoto wao kuambukizwa virusi vya HIV.
Maafisa
wa afya wamekana kuwa wanawake hao walifungwa uzazi kwa nguvu bila ridhaa yao .
Mawakili
wa wanawake hao wanasema kesi nyingine kama
hizo zimeripotiwa katika nchi nyingine katika ukanda huo.
Awali
mawakili wa wanawake hao walisema wateja wao waliambiwa na madaktari nchini Namibia kuwa
wangeweza tu kufanyiwa upasuaji iwapo wangekubali kufungiwa uzazi kwa wati huo.
Mawakili
hao wanasema kulazimishwa kukubaliana ni tofauti na kupatiwa taarifa muhimu ili
kukubalina na jambo hilo na kwa hiyo mamlaka za Namibia
zilikiuka haki za binadamu kwa wanawake hao.
Wizara
ya afya inakanusha kuwa ilitoa maelekezo kwa wanawake wanaoishi na virusi vya
HIV wafungiwe uzazi na kuongeza kuwa haikuwa inafahamu kuwa kuna mtu yeyote
amefungiwa uzazi bila ridhaa yao .
Nicole
Fritz, kutoka kituo cha Sheria cha Kusini mwa Afrika na hivyo kufungua kesi,
ameiambia BBC kuwa wanawake hao wamekuwa kwenye maumivu na hawajui nini
kitatokea.
"Mmoja
wa wanawake hao amekuwa kwenye uchungu kwa siku nne, uchungu ambao hauelezeki.
Wengine kati hao hawakujua hasa kile walichokuwa wakikubaliana nacho. Walidhani
ilikuwa ni sehemu ya utaratibu wa kufanyiwa upasuaji,"Alisema
"Hivyo
taarifa kuwa walikubaliana, hawakuelewa kilichokuwa kinaendelea, hawakujua
utaratibu ulivyokuwa na walikuwa wanakubaliana na nini, hawakuwa na taarifa za
kutosha kukubaliana. "
Mawakili
wanasema wana ushahidi kuwa wanawake wanalazimishwa kufungiwa uzazi nchini Swaziland na
baadhi ya maeneo ya Afrika Kusini, ambapo wanasema inawanyima wanawake hao haki
zao za kikatiba.
Kiasi
cha 13% ya watu wazima nchini Nambia wanaishi na virusi vya HIV kwa mujibu wa
UNAIDS.
Chanzo: BBC Swahili.
No comments:
Post a Comment