Saturday, July 28, 2012

Futari etu a leo...

Ndugu zangu,

Kwanza niwaombe radhi kwa kuchelewa kuwaletea futari ya leo. Nilikuwa katika kutekeleza tamko la Serikali la kujiandikisha kwa ajili ya kupata vitambulisho vya taifa, ambavyo juzi waziri wa mambo ya nje Benard Membe alivisifia sana kuwa ni vya kisasa zaidi ambavyo ukienda nchi yoyote vitatambulika na taarifa zako zitaonekana huko.

Kuna kitu nimekiona na nimejifunza katika zoezi hilo, nasikitika sikuwa na kamera yangu ambayo ingeniwezesha kupata matukio mengi, poleni mmekosa uhondo. Ila baada ya kuwaletea futari ya leo nitawahadithia nilichojifunza...

Futari ya leo itakuwa ni Mkate wa boflo (loaf) weka jam na siagi, chai ya maziwa, sambusa, katles na bhajia. Halafu weka biskuti na keki. Ukipata matunda aina tatu kama nanasi, embe na tikiti maji itakuwa umekamilisha mlo kamili.

Tafadhali usikariri kila siku kula vyakula vya urojourojo tu ni lazima ulizoeshe tumbo vakula va namna ningi iwezekanavyo, kula vyakula vya kawaida. Halafu kunywa na maji ya kutosha. Ahsanteni...

HAFIDH KIDO
DAR ES SALAAM, TANZANIA
0713 593894/ 0752 593894
28/07/2012

No comments:

Post a Comment