Baada ya tetesi za
majuma kadha, serikali ya Uganda
na Shirika la Afya Duniani, WHO, wamethibitisha kuwa ugonjwa wa Ebola umeibuka
magharibi mwa nchi hiyo.
Watu kama 13 wamekufa na
wengine kadha wanauguwa ugonjwa huo katika wilaya ya Kibaale. Chanzo cha
ugonjwa huo safari hii kingali kinachunguzwa.
Virusi vya Ebola havina
dawa wala chanjo ya kinga, na kati ya ishara zake ni homa, kutapika, na
kuhara.Ugonjwa huo ulizuka Uganda
miaka 12 iliyopita, na kuuwa watu zaidi ya 200.
Chanzo:http://www.bbc.co.uk/swahili/habari
No comments:
Post a Comment