Release No. 128
TAARIFA KWA VYOMBO VYA
HABARI
Julai 31, 2012
MECHI YA NGORONGORO
HEROES YAINGIZA MIL 12/-
Mechi ya kwanza ya
raundi ya pili kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Afrika kwa vijana chini ya
umri wa miaka 20 kati ya Tanzania (Ngorongoro Heroes) na Nigeria (Flying
Eagles) iliyochezwa juzi (Julai 29 mwaka huu) imeingiza sh. 12,901,000.
Fedha hizo zimepatikana
kutokana na watazamaji 3,377 waliokata tiketi kushuhudia pambano hilo
lililochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Sehemu iliyoingiza watazamaji wengi ilikuwa viti vya bluu na kijani ambapo 2,697 walikata tiketi kwa kiingilio cha sh. 3,000 kila mmoja. Viingilio vingine katika mechi hiyo vilikuwa sh. 5,000 kwa viti vya rangi ya chungwa, sh. 10,000 kwa VIP C na B, na sh. 15,000 kwa VIP A iliyoingiza watazamaji 21.
Mgawanyo wa mapato hayo
ni kama ifuatavyo; asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) ilikuwa sh.
1,967,949.15, gharama ya kuchapa tiketi sh. 2,250,000, gharama za waamuzi na
kamishna wa mechi hiyo sh. 760,000 na ulinzi na usafi kwa Uwanja wa Taifa sh.
2,350,000.
Malipo kwa Wachina
(Beijing Construction) sh. 2,000,000, asilimia 20 ya gharama za mchezo ni sh.
714,610.17, asilimia 10 ya uwanja sh. 357,305.08, asilimia 5 ya Shirikisho la
Mpira wa Miguu Afrika (CAF) sh. 178,652.54 na asilimia 65 ya Shirikisho la
Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) sh. 2,322,483.05.
Mechi ya marudiano ya michuano hiyo ambayo fainali zake zitafanyika mwakani nchini Algeria itachezwa Agosti 12 mwaka mjini Ilorin, Jimbo la Kwara, Nigeria.
PONGEZI KWA UONGOZI MPYA
SIREFA
Shirikisho la Mpira wa
Miguu Tanzania (TFF) linatoa pongezi kwa uongozi mpya wa Chama cha Mpira wa
Miguu Mkoa wa Singida (DOREFA) uliochaguliwa katika uchaguzi uliofanyika Julai
28 mwaka huu.
Ushindi waliopata
viongozi waliochaguliwa kuongoza chama hicho unaonesha jinsi wajumbe wa Mkutano
Mkuu wa SIREFA walivyo na imani kubwa kwao katika kusimamia mchezo huo mkoani
Singida.
TFF inaahidi kuendeleza
ushirikiano wake kwa Kamati ya Utendaji ya SIREFA chini ya uenyekiti wa
Baltazar Kimario ambaye amechaguliwa kwa mara ya kwanza.
Uongozi huo mpya una
changamoto nyingi, kubwa ikiwa ni kuhakikisha unaendesha shughuli za mpira wa
miguu mkoani Singida kwa kuzingatia katiba ya SIREFA pamoja na vyombo vya mpira
wa miguu vilivyo juu yake.
Pia tunatoa pongezi kwa
Kamati ya Uchaguzi ya SIREFA na Kamati ya Uchaguzi ya TFF kwa kuhakikisha
uchaguzi huo unaendeshwa kwa mujibu wa kanuni za uchaguzi za wanachama wa TFF.
Viongozi waliochaguliwa
katika uchaguzi huo uliofanyika Chuo Cha Maendeleo ya Jamii Singida ni Baltazar
Kimario (Mwenyekiti), Hussein Mwamba (Katibu Mkuu), Gabriel Gunda (Katibu
Msaidizi), Gabriel Mwanga (Mhazini), Hamisi Kitila (Mjumbe wa Mkutano Mkuu
TFF), Omari Salum (Mwakilishi wa Klabu TFF), Yagi Kiaratu na Dafi Dafi (wajumbe
wa Kamati ya Utendaji).
Nafasi za Makamu
Mwenyekiti, Mhazini Msaidizi na wajumbe wawili wa Kamati ya Utendaji zitajazwa
katika uchaguzi mdogo utakaofanyika baadaye.
MICHELSEN AITA 22 KAMBI
YA COCA-COLA
Kocha wa timu za Taifa
za vijana za Tanzania, Jakob Michelsen ameita wachezaji 22 kwa ajili ya
michuano ya kimataifa ya Coca-Cola itakayofanyika baadaye mwaka huu nchini
Afrika Kusini.
Baadaye watachujwa na
kubaki 16 ambao ndiyo watakaokwenda kwenye michuano ya Afrika Kusini. Wachezaji
waliochaguliwa wametokana na michuano ya Copa Coca-Cola iliyofanyika jijini Dar
es Salaam na mkoani Pwani kuanzia Juni 24- Julai 2 mwaka huu.
Wachezaji walioitwa ni
Abdulrahman Mandawanga (Dodoma), Abraham Mohamed (Mjini Magharibi), Ayoub Alfan
(Dodoma), Bakari Masoud (Tanga), Daniel Justin (Dodoma), Denis Dionis (Ilala),
Edward Songo (Ruvuma), Fikiri Bakari (Tanga), Hassan Kabunda (Temeke), Joseph
Chidyalo (Dodoma), Mutalemwa Katunzi (Morogoro) na Mwarami Maundu (Lindi).
Wengine ni Nankoveka
Mohamed (Ilala), Nelson Peter (Morogoro), Omari Saleh (Singida), Rajab Rajab
(Mwanza), Said Said (Kagera), Shiza Kichuya (Morogoro), Shukuru Msuvi (Temeke),
Tanganyika Suleiman (Kigoma), Tumaini Baraka (Kilimanjaro) na William John
(Ruvuma).
Pia Michelsen ameongeza
wachezaji saba kwenye kikosi cha Serengeti Boys ambacho Septemba mwaka huu
kitacheza na Kenya kuwania tiketi ya fainali za vijana wenye umri chini ya
miaka 17 za Afrika zitakazofanyika mwakani nchini Morocco.
Wachezaji walioongezwa kwenye kikosi hicho ambao pia wametoka kwenye Copa Coca-Cola ni Abdallah Baker (Mjini Magharibi), Abdallah Kheri (Mjini Magharibi), Calvin Manyika (Rukwa), Dickson Ambunda (Mwanza), Hassan Mganga (Morogoro), Miza Abdallah (Kinondoni) na Mzamiru Said (Morogoro).
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
No comments:
Post a Comment