Thursday, July 26, 2012

Futari yetu ya leo

Asalaam Alaykum,

Leo sitoongea mengi maana nina haraka kidogo natakiwa kuhudhuria kikao cha Wizara ya Fedha, kama muandishi si afisa. Msiogope bure wadau.

Tutapika, kalmati za sukari juu, Vibibi, viazi vitamu vya kuchemsha ama vya nazi, Mkate wa mchele (kumimina), chai ya maziwa. Tende ambazo hazijaiva sana, nyama ya kuchemsha tu ambayo utaila ikiwa kavu na matunda yoyote ambayo yatakuwa karibu nawe.

Usisahau kunywa maji mengi tafadhali ndugu yangu ili kuhakikisha chakula kinasagwa vizuri.

No comments:

Post a Comment