Katika siku za hivi
karibuni, kumejitokeza taarifa zenye tuhuma kadhaa dhidi ya Idara ya Usalama wa
Taifa. Taarifa hizo zimekuwa zikitolewa kwenye vyombo vya habari zikiihusisha
Idara hii na matukio ambayo yanaidhalilisha na kuzua maswali mengi kwa
wananchi.
Kati ya tuhuma hizo ni
tukio la kutekwa kwa Dr. STEPHEN ULIMBOKA, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari
na madai ya kufanywa kwa mipango ya kuwadhuru baadhi ya Viongozi wa Vyama vya
Upinzani. Gazeti moja la kila wiki limekuwa likurudia tuhuma hizo mara kwa mara
kwa madai kwamba ni
habari za uchunguzi na
kuihusisha Idara.
Idara inataka
kuwahakikishia wananchi kwamba taarifa hizo ni za UZUSHI NA UONGO ambazo zina nia
ya kuharibu jina na sifa ya Idara. Taarifa hizo zimekuwa zikiunganishaunganisha
vipande vya taarifa mbalimbali
ili kukidhi malengo
yaliyokusudiwa na wanaolitumia gazeti hilo .
Idara haikuhusika wala haihusiki na matukio yoyote yaliyotajwa katika tuhuma
hizo. Hivyo tunawaomba wananchi wazipuuze taarifa hizo.
Matukio yaliyotajwa
katika tuhuma hizo yanachunguzwa na Jeshi la Polisi ambacho ndicho Chombo
Chenye Dhamana, na kwa Maslahi ya Taifa si vizuri kuachia upotoshaji huo
uendelee.
Aidha, tunapenda
kuwahakikishia Watanzania kuwa uzushi na tuhuma zinazotolewa dhidi ya Idara
hazitatuvunja moyo bali zitatuunganisha na hivyo kutuimarisha katika azima yetu
ya kuhakikisha nchi yetu inaendelea kubaki salama kwa kushirikiana na wanachi
na Vyombo vingine vya Ulinzi na Usalama.
Imetolewa na Idara ya
Usalama wa Taifa,
Makao Makuu,
DAR ES SALAAM
26 Julai, 2012.
No comments:
Post a Comment