Mtume Muhammad (SAW), alisema: "Ukiona uchafu uondoe kwa mikono yako, ukishindwa utumie mdomo kukataza, ukishindwa basi utumie moyo kuhuzunika. Na moyo ni hatua ya mwisho na ya kidhaifu..... Ila hawa jamaa wamenifurahisha kweli...
Pata Habari kamili....
Kwa mujibu wa shuhuda wetu, waumini hao, wakiwa wamevaa kanzu huku wakitembea na bakora mkononi walichukua jukumu la kukodi Bajaj na kuzunguka maeneo mbalimbali jijini inapofanyika biashara hiyo haramu ya ukahaba.
Vijana
hao waliolenga kukomesha biashara hiyo hasa kipindi hiki cha mfungo walianzia
kwenye Barabara ya Shekilango inayokatiza kwenye viunga vya Sinza, Dar ambapo
kila kituo cha daladala kuanzia Afrika Sana hadi kwenye mataa ya Shekilango
waliwakuta machangu na kuwatandika viboko kabla ya kutua mitaa ya Mwenge.
Baada ya kufagiafagia Sinza kwa kuwaadabisha wanawake hao ndipo zoezi likahamia mitaa ya Kinondoni ambapo nao walipokea bakora za kutosha huku wengine wakitoka nduki.
Kwa mujibu wa vijana hao, walifikia hatua ya kufanya zoezi hilo baada ya muumini mmoja wa kiume kukatiza maeneo ya Corner Bar, Afrika Sana na kuvutwa kisha kuchezewa nyeti na makahaba na kusabisha kuharibika kwa swaumu yake.
Ilielezwa kuwa
baada ya kukutwa na kimbembe hicho, ilibidi muumini huyo kukatiza safari yake
ya kwenda kuswali msikikini mishale ya saa 2:00 usiku.
lisemekana kuwa aliporudi nyumbani alitawadha na kufunga safari
nyingine ya msikitini na alipofika kwenye nyumba hiyo ya ibada ndipo
akawasimulia waumini wenzake ambao nao walikasirishwa na kitendo hicho hivyo
wakapanga kuvamia maeneo yote ya biashara hiyo ili kuwashikisha adabu.
Waandishi wetu,
wakiwa kwenye mishemishe zao za kutafuta habari mishale ya saa 5 usiku
waliwashuhudia waumini hao wapatao saba wakishuka kwenye Bajaj nyeusi maeneo ya
Sinza wakiwa na bakora mikononi kisha kuwavaa machangu hao na kuwatandika.
Wakati
wakitekeleza zoezi hilo, jamaa hao walisikia wakiwaambia: “Sisi tupo kwenye
swaumu nyiye mnatutega, ala!”
Waumini hao
waliongeza kuwa makahaba hao wamekuwa hawaheshimu mwezi huu Mtukufu wa Ramadhan
ndiyo maana wanaendeleza biashara yao hiyo ya aibu.
www.globalpublishers.info
No comments:
Post a Comment