Friday, July 27, 2012

A to Z story ya Erick Shigongo na Jose Chameleon hii hapa, lakini nimechanganya lugha mbili, kiswahili na kizungu ili kuhakikisha sizidishi wala sipunguzi walichozungumza wadau kwa kauli zao.

 Hapa akiwa ubalozi wa Tanzania nchini Uganda. Hapa nimeshaingia sana nyumba hii, ila chamoto walikiona wenzetu wanajua kudai haki bwana.

Dr Chameleon akiwa na mkuu wa jeshi la Polisi Uganda Kale Kaihura, jambo limekwisha....

(Tunaanza na hii ambayo ni habari imetolewa leo katika gazeti la Nipashe)

Mwanamuziki nyota wa Uganda, Joseph Mayanja maarufu kama Jose Chameleon, jana alipiga kambi kwenye ubalozi wa Tanzania nchini Uganda akishinikiza kurejeshewa pasi yake ya kusafiria iliyoshikiliwa na promota wa muziki wa Tanzania.

Akiongea na Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) jana msanii huyo alisema alitua nchini Tanzania kufanya onesho Julai 7, 2012 baada ya wakala wake kupokea dola 3,000.

Chameleon alisema baada ya onesho hilo alishangaa kuona pasi yake ya kusafiria ikishikiliwa na promota huyo, hivyo kuhatarisha safari yake ya kwenda kutumbuiza kwenye michuano ya Olimpiki nchini Uingereza.

Msanii huyo alisema kuwa baada ya kuona pasi yake inachelewa kumfikia, aliondoka katika ubalozi huo na kutafuta pasi ya muda iliyomwezesha kwenda nchini Uingereza.

Akijibu hoja za Chameleon, Balozi wa Tanzania nchini Uganda, Dk. Ladislaus Komba, alisema alipokea malalamiko ya msanii huyo na kuanza kuyafanyia kazi lakini alimshangaa msanii huyo kusafiri kwenda Uingereza kwa pasi ya muda wakati pasi yake ilikuwa tayari imeagizwa kutoka Dar es Salaam na ilikuwa njiani.

Julai 7 mwaka huu Chameleon alifanya onesho kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam katika Tamasha la Matumaini lililolenga kukusanya pesa kwa ajili ya ujenzi wa hosteli za wanafunzi wa kike katika shule mbalimbali za sekondari jijini Dar es Salaam, ambalo Diamond pia alitumbuiza na waigizaji Wema Sepetu na Jacqueline Wolper walipambana ulingoni katika ndondi za hisani.
Chanzo: IPP Media



(Halafu inafuata hii, haya ni maneno yake mwenyewe Chameleon aliyaandika katika ukurasa wake wa facebook. Sijazidisha wala sijapunguza).

DR. JOSE Chameleone


I AM VERY DISAPPOINTED!

I WAS HIRED BY GLOBAL PUBLISHERS A TANZANIAN COMPANY, TO PERFORM AT THE NATIONAL STADIUM ON THE 7th July 2012.

I PERFORMED AS THE CONTRACT AGREED! ON SUNDAY 8th ONE ERIC SHIGONGO THE CEO GLOBAL PUBLISHERS CONFISCATED MY PASSPORT ALLEGING MY MANAGER HAD SWINDLED HIS 3500$, WHICH IN REAL SENSE WAS SWINDLED BY A KAMPALA CONMAN CALLED GEORGE. 

I WAS ASSISTED BY THE UGANDAN EMBASSY IN DAR EL SALAAM, WHO GAVE ME A TEMPORARY DOCUMENT TO RETURN ME HOME. 
ON RETURN TO UGANDA I HUNTED FOR THE CONMAN, ARRESTED HIM AND HANDED HIM OVER TO POLICE, WHO FREED HIM ON CONDITIONS I DON'T KNOW!

I EXPLAINED TO THE TANZANIAN AMBASSADOR AT THE TANZANIAN HIGH COMMISSION IN UGANDA FOR ASSISTANCE BUT SEEMS IN VAIN.

I HAVE UPCOMING PERFORMANCES IN

SOUTH AFRICA, ENGLAND,BELGIUM, NORWAY,SWEDEN, CANADA ETC!

SO IS ERIC SHIGONGO ABOVE THE LAW TO KEEP MY PASSPORT ILLEGALY?

AM I LIABLE TO HIS NEGLEGANCE THAT HE TRUSTED A CONMAN?

IS IT FAIR THAT AN UNAUTHORIZED TANZANIAN CITZEN CAN KEEP MY PASSPORT FOR OVER A MONTH?

I NEED ADVICE


Akaendelea hivi:

ERIC SHIGONGO AM BOUND TO MAKE YOU AN EAST AFRICAN CELEBRITY GOR TAKING THE LAW THE WAY YOU WANT! WE ARE PLANNING EAST AFRICA UNION AND U ARE PROMOTING YOUR SELFISH UNION! Damn
Akaendelea tena:I AM AT THE TANZANIAN HIGH COMMISSION IN DEMOSTRATION FOR THE CONFISCATION OF MY PASSPORT BY A TANZANIAN ILLEGALY ERIC SHIGONGO I NEED MY FREEDOM TO TRAVEL AS A UGANDAN!

I NEED MY PASSPORT BACK ASAP!

FOR GOD AND MY COUNTRY UGANDA.NA TENA:
Woken up! AM NOT GOING TO GO BACK TO MY HOUSE! AM GOING TO SLEEP AT THE TANZANIAN HIGH COMMISSION UGANDA UNTIL MY BROTHER FROM TANZANIA SURRENDERS BACK MY PASSPORT TO UGANDA GOVERNMENT THAT OWNS IT.HE IS HOLDING IT ILLEGALLY- IF NO BODY IS THERE FOR MY RIGHT AND JUSTICE LET ME ASK FOR IT MYSELF! 

I AM DEMONSTRATING AGAINST INJUSTICE
AND WANT ERIC SHIGONGO TO RESPECT MY COUNTRY! 

FOR GOD AND MY COUNRTY I DECLARE.

Erick Shigongo huyu mmiliki wa kampuni ya Global Publishers wakati wa tamasha la matumaini Uwanja wa Taifa.
(Halafu haya ni majibu ya Erick Shigongo)

SHIGONGO: Watanzania wafahamu wakati wa kudharauliwa na Wakenya na Waganda umepita, Chameleone nimemlipa hela mara mbili lakini aliruka kuhusu ya mara ya kwanza ambayo ni USD 3500, KIDUMU shahidi.. alikutana na Agent na Chameleone mwenyewe Uganda.


Aidha,wakati Shigongo alipokuwa akizungumza na Fatma wa Clouds FM maarufu Dj Fetty alisema Cameleon alipanga kumdhulumu maana alishampatia dola 3500 za kimarekani lakini bado akakana kuwa hajapatiwa hata senti, kwa kuwa zilikuwa zimebakia siku mbili kufanyika tamasha na yeye alikuwa ameshatangaza uwepo wake katika tamsaha hivyo aliamua kumpatia hizo pesa alizotaka za dola 8000 za kimarekani.


Hivyo akaamua kuizuia pasi yake ya kusafiria ili aweze kumrudishia pesa zake baada ya tamasha kuisha, maana anataka kuwaonyesha watu wa nchi jirani kuwa watanzania si wapole tena maana walizidi kuwadhulumu na sasa wameshaamka.

No comments:

Post a Comment