MARUPURUPU ya wabunge
ikiwamo mishahara imeongezwa kutoka Sh7.4 milioni kwa mwezi hadi takriban
Sh11milioni kwa mwezi, hatua ambayo imeibua mjadala mwingine mzito miongoni
mwao.
Tangu mwaka jana,
wabunge wamekuwa katika vita ya kupokea au kutopokea posho ya vikao ambayo
imekuwa ikikolezwa na Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe ambaye
alizikataa akisema mbunge anapokuwa kazini hahitaji kulipwa.
Hata hivyo, uchunguzi wa
gazeti hili umebaini kwamba sasa vita kubwa ipo katika marupurupu mapya ambayo
pamoja na kuchanganya na mshahara yanafikia Sh11milioni kwa mwezi.
Spika wa Bunge, Anne
Makinda alipoulizwa jana alithibitisha kuhusu kuongezeka kwa malipo jumla ya
wabunge kwa mwezi lakini akasema hafahamu kiwango halisi kilichoongezwa.
Makinda alisema nyongeza
iliyopo siyo kwa wabunge tu, bali watumishi wote wa Serikali na ilitangazwa na
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma), wakati wa
Bajeti ya Ofisi hiyo kwa mwaka 2012/13.
“Hiyo nyongeza siyo tu
kwa wabunge, bali ni kwa watumishi wa Serikali. Tena hiyo ilitangazwa na Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma). Sasa ukiniuliza kiasi
gani hapo ndipo sielewei, ila najua nyongeza ipo,” alisema Spika.
Lakini, vyanzo kutoka
ndani ya Bunge vilisema kwamba nyongeza hiyo ambayo tayari imeingia katika
mshahara wa Julai ni Sh3.6milioni, hivyo kufanya jumla ya fedha anazochukua
mbunge kufikia kiasi hicho cha Sh11milioni.
“Hiyo ni vita, kuna
wabunge wana hasira kweli hawataki wananchi wajue kama
marupurupu yameongezeka.
Wanaona wananchi wakijua
itakuwa ni tatizo kubwa, watapigiwa kelele lakini nyongeza hiyo ipo. Tayari
wengine wamechukua tangu Ijumaa,” kilisema chanzo kimoja kwa sharti la
kutotajwa jina gazetini.
Hata hivyo, kwa mujibu
wa chanzo hicho, baadhi ya wabunge kutoka kundi la wanaopinga posho kwa wabunge
wamepinga pia nyongeza hiyo wakitaka fedha hizo zielekezwe katika sekta
nyingine za kijamii.
Marupuru ya sasa
Hadi mwezi uliopita,
mbunge alikuwa akipokea Sh7.4milioni kwa mwezi ambazo kati ya hizo Sh2.5milioni
ni kwa ajili ya mafuta, Sh2.3 mshahara, Sh170,000 kwa ajili ya mshahara wa
dereva, 100,000 kwa ajili ya katibu wa mbunge na posho ya jimbo.
Hata hivyo, katika
nyongeza hiyo ya sasa haijawekwa wazi kwamba kiasi gani ni kwa ajili ya
mshahara, fedha za mafuta ya gari la mbunge, za dereva, katibu na za posho ya
jimbo na tayari baadhi ya wabunge wameanza kufuatilia mchanganuo wa nyongeza
hiyo.
Chanzo:
No comments:
Post a Comment