Mmarekani aliyetuhumiwa kwa kujaribu kujiunga na kundi
lenye msimamo mkali la Kiislam la al-Shabab nchini Somalia amekiri mashtaka yake
kwenye mahakama Marekani.
Shaker Masri, 28, alikamatwa Agosti 2010 akijiandaa kusafiri
kwenda Somalia kukijunga na al-Shabab, kwa mujibu wa mwendesha mashtaka wa
Marekani.
Marekani na Uingereza wanaliona kundi hilo likijihusisha na
al-Qaeda, kuwa ni kundi la kigaidi.
Katika
makubaliano ya kukubali mashtaka, Masri amekubali kutumikia kifungo chini ya
miaka kumi gerezani.
Alikiri
kupanga njama za kukusanya fedha alizohitaji kujzitumia katika jihadi ama Somalia au Afghanistan .
Amehukumiwa
kifungo za miaka 15 gerezani.
Masri
alizaliwa Alabama na kuishi Chicago kabla ya kukamatwa saa chache
hajaondoka nchini.
Amekuwa
akijieleza kama wakala wa FBI wa siri na
amekuwa akizungumzia kuhusu kuwalenga ‘makafiri’
Kufuatia
kukamatwa kwake alishtakiwa kwa kujaribu kusaidia kwa mali kundi la
kigaidi, akijaribu kuwapa msaada kwa kutumia silaha za maangamizi.
Taarifa
kamili za kukiri kwake hazijatolewa kwa umma.
Al-Shabab
wanaamini kuwa ikiwapata wasomali wenye asili ya Kimarekani kushiriki katika
kujitoa muhanga nchini Somalia
na maafisa wa Marekani sasa wana wasiwasi wa kuwepo shambulio ndani ya
Marekani.
Raia
kadhaa wa Marekani wamekamatwa katika miaka ya karibuni wakijaribu kushiriki au
kuunga mkono vita vya zaidi ya miongo miwili iliyopita.
Shaker
Masri atahukumiwa rasmi mwezi Oktoba 16.
Chanzo: BBC Swahili.
No comments:
Post a Comment