Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeonyesha wasiwasi
wake juu ya kuongezeka kwa biashara ya dawa za kulevya Guinea-Bissau
tangu mapinduzi yatokee mwezi April.
Limetaka viongozi nchini humo kurejesha utawaa wa kikatiba.
Imekuwa
ndio kitovu cha magenge ya kupitishia cocaine kutoka Latin
America mpaka Ulaya, ikituhumiwa kushirikiana na maafisa wa jeshi.
"Wajumbe
wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wamelaani kitendo cha jeshi kuingilia
siasa na kuonyesha wasiwasi wake kuhusu taarifa za kuongezeka kwa usafirishaji
wa dawa kuongezeka tangu April 12 mapinduzi yalipotokea." Baraza la
Usalama la Umoja wa Mataifa lilisema katika mkutano wake New York .
Limesema
lilikuwa linaangalia uwezekano wa mkutano wa kimataifa kuzungumzia ni kwa namna
gani watafanikiwa kurejesha utawala wa kidemokrasia nchini Guinea Bissau.
'Ushawishi'
Mwezi
Mei , Baraza hilo
liliweka vikwazo vya kusafiri kwa viongozi wa mapinduzi na wanaowaunga mkono.
Jeshi
limekubali mazungumzo yasimamiwe na ECOWAS, kurejesha nchi katika utawala wa
demokrasia lakini limeshindwa kufanya hivyo.
Mwaka
2010, Marekani iliwashutumu wanajeshi kutoka Guinea-Bissau , wakiwemo mkuu wa
jeshi la majini Jose Americo Bubo Na Tchuto, kwa kuhusika na dawa za kulevya.
Katika
sheria ya Ushawishi wa Dawa za kulevya , vikwazo vya kifedha viliwekwa.
Hakuna
wa kuchaguliwa kwa karibu miaka arobaini sasa ya uhuru ambaye amewahi kumaliza
muda wake wa uongozi nchini Guinea-Bissau .
Chanzo: BBC Swahili
No comments:
Post a Comment