WAKATI
wabunge wakitoa tuhuma nzito dhidi ya wenzao wanaodaiwa kujihusisha na ufisadi
ndani ya Shirika la Umeme Tanzania
(Tanesco), imebainishwa kuwa wabunge wenye tabia hiyo ni watano, watatu kutoka
chama tawala CCM na wawili upinzani.
Habari
zilizopatikana jana mjini Dodoma
zimeeleza kuwa baadhi ya wabunge hao wanatoka katika Kamati ya Bunge ya Nishati
na Madini, huku wengine wakitoka Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya
Umma.
Kwa mujibu
wa taarifa hizo, wabunge hao wamedaiwa kuwa wamekuwa wakitumia nafasi zao
za ubunge na ujumbe wa kamati kufanya biashara na Tanesco na kutetea mafisadi
ndani ya shirika hilo
la umma.
Gazeti hili
limefanikiwa kupata majina ya wabunge hao, ambayo leo hatutayataja kwa sababu
za kitaaluma.
Baadhi ya
wabunge waliochangia hoja hiyo bungeni juzi na jana walisema kuwa, wanawafahamu
wabunge hao kwa majina, lakini hawapendi kuwataja kwa kuwa siyo wakati mwafaka.
Moto wa
kutaka kutajwa kwa majina ya wabunge hao ulikolezwa jana na Mbunge Vita Kawawa
wa Namtumbo(CCM) aliyeomba Mwongozo wa Spika, akitaka jambo hili lijadiliwe na
Bunge na kupendekeza kuwa, Kamati za Bunge zinazotuhumiwa kwa rushwa zivunjwe.
“Waheshimiwa
wabunge wamejadili suala hili kwenye wizara, lakini kwa mujibu wa kifungu cha
55 (3)f mbunge au waziri anaweza kutoa hoja ili jambo fulani lijadiliwe.
Sasa naomba kutoa hoja ya kujadili suala hilo ,"
Kawawa alisema.
Aliliomba
pia Bunge likubali kuivunja na kuiunda upya Kamati ya Nishati na Madini na
kamati nyingine zilizolalamikiwa kwa rushwa. Hoja hiyo iliungwa mkono na
wabunge.
Baada ya
hoja hiyo kuungwa mkono Spika wa Bunge, Anne Makinda alisimama na kukubali hoja
hiyo ya Kawawa na kutangaza kuivunja Kamati ya Nishati na Madini.
Spika
Makinda alisema ameiagiza Kamati ya Haki, Kinga na Maadili ya Bunge kutengeneza
kanuni za kuwadhibiti wabunge wenye tabia hiyo ya kupokea rushwa kutoka kwa
watu mbalimbali ili kutimiza matakwa yao
binafsi. Soma zaidi....http://www.mwananchi.co.tz
No comments:
Post a Comment