Thursday, July 26, 2012

Mwalimu wa mwisho miongoni mwa walimu waliowahi kumfundisha hayati baba wa Taifa amezikwa leo kijijini Busegwe.




Mwalimu James Irenge, ambaye ni mwalimu wa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, amezikwa leo katika kijiji alichozaliwa cha Busegwe- Nyanza wilayani Butiama, huku mazishi yake yakihudhuriwa na viongozi wa Serikali akiwemo Waziri Mkuu Mizengo Pinda.

Mzee Irenge fariki dunia jumatatu usiku kutokana na umri mkubwa na maradhi ya hapa na pale.

Mzee Irenge, aliyekuwa na umuri wa miaka zaidi ya 120, alimfundisha Mwalimu Nyerere katika Shule ya Mwisenge, kati ya mwaka 1934-1936.


Hadi mauti yanamfika, licha ya umri wake mkubwa, bado alikuwa na uwezo wa kusoma na kuandika mwenyewe bila kutumia miwani.

Wiki kadhaa zilizopita, aliandika barua yake ya mwisho kwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda, wiki iliyopita akimshuru kwa kumwezesha kumlipa fedha za dawa na chakula; mambo yaliyokuwa kilio chake cha siku nyingi.

Mwalimu Irenge mara kadhaa alikuwa akilalamika kwamba tangu alipostaafu ualimu miaka ya 1970 hakupata kulipwa mafao yake, na kiinua mgongo.

Kifo chake, kinahitimisha uhai wa walimu wa Mwalimu Nyerere. Mwalimu mwingine, Daniel Kirigini, alifariki dunia mwanzoni mwa miaka ya 2000.

Mwalimu Irenge Ameacha mjane, watoto 12, wajukuu 30 na vitukuu 15.

No comments:

Post a Comment