Sunday, July 29, 2012

Tanga wavunja rekodi ushiriki bongo star search.... Yachukua washiriki sita badala ya watano.

kama kawaida yake Salama jabbir hakosi kituko cha kufanya kila mkoa anaoenda.....

Mwaka huu tanga imeonekana kutia fora katika mchujo wa kupata washiriki wa shindalo la kuimba la bongo star search 2012. Maana walijitokeza watu 800 halafu wote wakali. Majaji wakaamua kuvunja utaratibu na kuchukua wahiriki 6 badala ya 5 wa desturi. maana hawakujua wamchukue yupi wamuache yupi.

Mwaka huu mikoa iliyowahenyesha majaji hao Madam Rita, Master J na Salama jabir, ni mikoa miwili mpaka sasa. Mwanza ambako walijitokeza washiriki wengi kuliko mikoa yote mpaka ikawapasa kufanya kazi kwa saa nyingi zaidi takriban saa 20 kutafuta washiriki watano.

Na Tanga ambapo mbali ya kujitokeza washiriki wengi lakini ilionekana kuna vipaji vingi mpaka ikawa ni kazi ngumu kuacha yupi na kuchukua yupi, kifupi Tanga imekuwa kama timu ya mpira ya Brazil. Hujui umchukue yupi umuache yupi wote wakali..... habari ndiyo hiyo....

No comments:

Post a Comment