Huyu ni Khamis Kiiza mfungaji wa bao la kwanza.....
Ndugu zangu,
Kawaida napenda kutoa kila ninachojifunza mahali ninapokwenda. Mungu ameniwezesha kushuhudia fainali nzuri za kombe la Kagame, na nimefurahishwa sana maana niliona mpira mzuri wa Yanga pamoja na Azam.
Dakika za awali Azam walianza vizuri na kucheza mpira uliotulia na kuonana vizuri sana mpaka mashabiki wa Simba na Azam wakawa wanapata raha sana.
Ila mambo yalibadilika baada ya Khamis Kiiza kutumbukiza mpira nyavuni kimaajabu na kumuacha mdomo wazi golikipa wa Azam Dida, katika dakika ya 44 ya kipindi cha kwanza.
Kipindi cha pili hali ilikuwa tulivu maana Yanga walikuwa wakicheza mpira wa kujihami na Azam wakawa wanatafuta goli kwa nguvu bila mafanikio. Dakika ya sabini kocha wa Azam akamuingiza Mrisho Ngassa, na kumtoa Kipre Tche Tche, lakini uamuzi huo haukupokewa kwa furaha na mashabiki wa Simba maana walikuwa wakishabikia Azam na wanamtuhumu Ngassa kuwa na mapenzi ya dhati na timu ya Yanga ingawa ni mchezaji wa Azam, lakini alijitahidi kuubadili mchezo na kuonekana kuwa na matumaini ya kusawazisha.
Lakini hali ilikuwa mbaya baada ya Said Bahanuzi, kuingiza mpira wavuni katika hali ambayo haikutarajiwa na wengi baada ya dakika tisini kuisha na kuongezwa dakika tatu za mwamuzi...
Hali hiyo iliwavunja nguvu mashabiki wa Simba na Azam hivyo wengi kuanza kuondoka maana walijua kuwa wali ulishaingia mafuta ya taa hivyo kuunusuru ni suala gumu.
Kitu kilichonikera katika mchezo huo ni utaratibu mbovu wa kukata tiketi. Kuna urasimu mkubwa sana kama foleni zisizofuata utaratibu na kufichwa kwa tiketi za bei ya chini huku wakilazimisha kuuza tiketi za bei ya juu ili wapate faida ya haraka.
Hata hivyo naipongeza Azam kwa kuchukua kikombe hicho kwa mara ya tano, lakini mara hii wamevchukua mara ya pili mfululizo hivyo imebaki mara moja tu ili wabaki nacho kabisa....
No comments:
Post a Comment