SAKATA la wabunge
kuhusishwa na rushwa limeingia sura mpya, baada ya Naibu Kiongozi wa Upinzani
Bungeni, Zitto Kabwe kuhojiwa na chama chake cha Chadema kwa saa tatu jana.
Wakati Zitto akihojiwa,
kambi rasmi ya upinzani bungeni, iliwataja wabunge saba wa CCM na kueleza kuwa
ndiyo wanaolichafua Bunge kwa kujihusisha na mambo yenye maslahi binafsi wakiwa
watumishi wa umma.
Kadhalika, Naibu Spika
wa Bunge, Job Ndugai alisema kwamba Taasisi ya Kuzuia na Kupamba na Rushwa
(Takukuru) ilikuwa ikiendelea kuwahoji baadhi ya wabunge kuhusu tuhuma za
rushwa na kwamba uchunguzi ukikamilika taarifa zitawekwa wazi.
Zitto ambaye pia ni
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC) na Naibu
Katibu Mkuu wa Chadema, jana aliandika katika ukurasa wake wa mtandao wa
Tweeter kwamba alihojiwa na Sekretarieti ya chama chake kutokana na tuhuma za
rushwa zinazowagusa badhi ya wabunge.
Katika maelezo yake,
Zitto alisema aliiambia sekretarieti ya chama hicho kwamba Chadema kifanye
uchunguzi ili kubaini ukweli wa suala hilo na kwamba yuko tayari kuwajibika
ikiwa itathibitika kwamba alihusika kula rushwa.
“Kwa saa tatu
nimejieleza mbele ya sekretariati ya chama kuhusu tuhuma za rushwa dhidi yangu.
Niliomba kutaka kutoa maelezo kwa Katibu Mkuu, nimekiomba chama kufanya
uchunguzi na ikibainika hatua zichukuliwe,” inasomeka sehemu ya taarifa hiyo
kwenye Tweeter.
Lissu ataja wengine
Kwa upande wake,
Mnadhimu Mkuu wa kambi hiyo, Tundu Lissu aliwataja wabunge wa CCM ambao
wanatuhumiwa kuwa ni Nasir Abdallah (Korogwe Mjini), Mariam Kisangi (Viti
Maalumu), Vicky Kamata (Viti Maalumu) na Charles Mwijage (Muleba Kaskazini)
ambao hata hivyo, wote wamekanusha madai hayo.
Habari zaidi: http://www.mwananchi.co.tz/habari
No comments:
Post a Comment