Familia ya kifalme imeukaribisha mwenge wa Olimpiki katika
Kasri la Buckingham katika siku ambapo umati mkubwa wa watu ulikusanyika mjini London kushuhudia mkondo wa mwisho wa safari ya mwenge huo
mjini London .
Mwenge huo kadhalika uliwasilishwa
Baada ya tetesi kuzuka kuhusiana na maandalizi
ya michezo hiyo, waziri mkuu wa Uingereza David Cameron amesema michezo ya
mwaka huu itathibitisha kuwa Uingereza ina uwezo wa kufanya maandalizi kabambe.
Lenye
Ijumaa ndiyo siku ya ufunguzi rasmi wa mashindano yatakayopeperushwa moja kwa
moja kote duniani.
Bwana Cameron ametetea maandalizi ya mashindano hayo baada ya mgombea wa kiti cha urais nchini Marekani Mitt Romney kusema kwenye mahojiano katika runinga ya NBC kwamba kuna matatizo katika usalama na tishio la mgomo wa maafisa katika maeneo ya mipakani.
Lakini
baadaye bwana Romney alitabiri kuwa mashindano ya Olimpiki mjini London yatakuwa yenye mafanikio baada ya kukutana na
waziri mkuu huko Downing Street .
Hapa
Bw. Cameron aliukaribisha mwenge huo wakati uliposimama kwa muda ukiwa njia
kuelekea Kasri la Buckingham.
Mwanamfalme
William, mkewe na mwanamfalme Harry walikuwepo kuwakaribisha waliokuwa
wakiiperusha mwenge huo kabla ya kupelekwa Hyde Park .
Meya
wa mji wa London Boris Jonnson akizungumza mbele ya umati mkubwa wa watu 60,000
waliojitokeza kushuhudia sherehe hiyo aliwatakiwa kila la heri na kusema
''mashindano ya London
yatakuwa ni ya kukata na shoka.''
Lakini
pia alizungumzi mzozo uliokuwepo awali aliposema mbele ya umati huo: "kuna
mtu anayeitwa Mitt Romney ambaye anataka kujua ikiwa tuko tayari. Tuko tayari?
Ndiyo tuko Tayari!"
No comments:
Post a Comment