Washiriki wa warsha ya wapiga picha kutoka nchi wanachama wa Jumuiya ya
Afrika Mashariki wakiwa katika picha ya pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa EAC
anayeshughulikia Shirikisho la Kisiasa Dr Julius Rotich (aliyeketi wa pili
kushoto) mjini Arusha jana. Kushoto kwake ni Kaimu mkuu wa mpango wa EAC-GIZ
and kulia ni Mkuu wa Idara ya Habari EAC Owora Othieno. Kulia kabisa
aliyesimama ni mratibu wa mafunzo wa EAC Sukhdev Chhatbar.
Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya
Afrika Mashariki (EAC), anayeshughulikia Shirikisho la Kisiasa,Dkt. Julius Rotich(akifafanua jambo kwa waandishi juu ya Mafunzo ya
Upigaji picha ‘EAC-GIZ Master Class Photographers Training’
Mpiga picha mahiri kutoka Tanzania na mmiliki wa blogu ya 'father kidevu' Mroki Mroki, akizungumza na wanahabari wakati wa
mafunzo ya siku tatu ya upigaji picha yajulikanayo kama ‘EAC-GIZ Master Class Photographers Training’ yaliyoanza
Julai 23-26, 2012 mjini Arusha.
Mkufunzi Mkuu wa Upigaji picha ambaye pia ni Mpigapicha kutoka Ujerumani
ambaye anafanya shughuli zake nchini Kenya, Hartmut Fiebig akitoa
maelekezo kwa wapigapicha.
Washiriki kutoka nchi wanachama za Afrika ya Mashariki wakiwa darasani ambapo kila nchi ilitoa washiriki wawili kuhakikisha mafunzo hayo yanaleta udugu na muingiliano mzuri kutoka nchi tano za jumuiya hiyo.
No comments:
Post a Comment