Polisi wa Kenya wanasema kuwa wanaendelea na uchunguzi,
juu ya mauaji ya balozi mpya wa Venezuela nchini humo, ambaye aliuwawa Ijumaa.
Olga Fonseca, aliyeanza kazi Kenya kati ya mwezi Julai,
alikutiakana ameuwawa nyumbani kwake, na watu sita wamekamatwa hadi sasa.
Watu
hao sita wamekamatwa siku mbili tu baada ya balozi huyo kupatikana amefariki
nyumbani kwake.
Siku
ya Ijumaa, polisi walisema kuwa maiti ya Bi Olga Fonseca ilipatikana kitandani
mwake lakini sababu za kuuwawa kwake hadi sasa hazijulikani.
Bila
ya kutoa maelezo zaidi, polisi wamesema kuwa wanawashikilia watu sita kuhusiana
na kifo cha balozi huyo.
Taarifa
kutoka wizara ya maswala ya njee ya Kenya
imesema kuwa wafanyikazi katika makaazi ya balozi huyo waliwasilisha malalamiko
yao kwa polisi
baada ya kufutwa kazi hivi majuzi.
Inadaiwa
kuwa bi Fonseca aliwafuta kazi baada ya wao kukataa kuondoa malalamiko kuhusu
madai ya kunyanyaswa kijinisia na mtangulizi wa balozi huo.
Hata
hivyo polisi wamesema wanachunguza madai hyao.
Wakati huohuo
Mashirika yasiyokuwa ya serikali katika Jamhuri ya
Demokrasi ya Congo, yanasema kuwa wanajeshi wa Uganda wameingia Jamhuri ya
Demokrasi ya Congo, kupigana pamoja na jeshi la huko dhidi ya wapiganaji
waitwao M23.
Mashirika hayo
yanasema magari ya deraya sita, yaliyojaa wanajeshi yamevuka mpaka kutoka Uganda ,
na kuingia jimbo la Kivu Kaskazini.
Jeshi
la Uganda
limekanusha tuhuma hizo.
Mataifa
kadha ya magharibi yamesimamisha msaada kwa Rwanda ,
baada ya ripoti ya Umoja wa Mataifa kusema kuwa Rwanda
inalisaidia kundi la wapiganaji la M23 -- tuhuma ambazo zinakanushwa na Rwanda .
Chanzo: BBC Swahili
No comments:
Post a Comment