Sunday, July 29, 2012

Mukoba aivimbia Serikali, adai mgomo upo palepale siku ya jumatatu tarehe 30.

Rais wa chama cha walimu Tanzania Gratian Mukoba akizunumza na wanahabari kuhusu mgomo wa walismu siku ya Jumatatu. Mbali ya Serikali kutangaza mgomo huo ni batili kwani kesi ipo mahakamani.


Rais wa chama cha walimu Tanzania (C.W.T)Gratian Mukoba (katikati) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo makao makuu ya chama cha walimu Tanzania (CWT) jijini Dar es salaam juu ya Baraza la C.W.T ambalo limetoa notisi ya saa 48 kwa serikali kuanzia jana tarehe 27 Julai 2012 saa 8.00 mchana baada ya saa hizo walimu wataanza mgomo rasmi kuanzia siku ya jumatatu tarehe 30 Julai 2012.

Kauli hiyo imekuja huku Serikali kupitia kurugenzi ya mawasiliano Ikulu ya jijini Dar es Salaam ikiwa imeshatoa kauli kupinga kuwepo kwa mgomo huo na kusema ni batili na atakae kaidi kauli hiyo kukiona.
Waalimu waliamua kupiga kura ili kufanya uamuzi huo wa mgomo ambapo kura asilimia 95.7 za walimu wanaofundisha katika shule za awali, msingi, sekondari, maafisa walioko kwenye ukaguzi  wa shule na wanafunzi wa vyuo vya ualimu na maendeleo ya jamii. Wanachama wote wameunga mkono mgomo kulia ni  Makamu wa Rais C.W.T. Honoratha Chitanda na kushoto ni Mweka hazina wa chama hicho Mohamed Utaly. 

Mukoba amewataka walimu kushiriki mgomo huo halali ambao umeitishwa na chama kwa mujibu wa sheria nakusema mgomo huo auhusiani na zoezi la sensa.
Chanzo: Said Powa blog












No comments:

Post a Comment