Monday, July 30, 2012

Futari ya leo,

Asalam alaykum,

Alhamdulillah tyumemaliza salama kumi la kwanza ambalo limeitwa la Rehma, kwa maana Rehema za Mungu zinamshukia kila mwenye kuzihitaji. Na sasa tunaingia katika awamu ya pili ambayo ni kumi la Maghufira, Maana yake kila mwenye kuhitaji msamaha wa Mungu ndiyo wakati wake huu kujipinda.

Futari yetu ya leo tutapika vitu vichache ambavyo havitakufanya usumbuke sana. Na wengi wataona kama haifai kwa futari, lakini pia inaruhusiwa siku moja moja kupika vitu vichache ambavyo vitakufanya uwe na muda wa kutosha kufanya mambo menine.

Tutapika chips na samaki wa kukaanga. Halafu matunda ya kutosha kama machunwa, apple (tufaha) na tikiti maji (water melon) ukiongeza na parachichi (avocado). Nadhani mlo wetu utakuwa umekamilika kwa leo. Usisahau kuweka salad (kachumbari) nyingi ambayo haijachanganywa na ndimu wala chumvi ili kupoteza ubora wake.


No comments:

Post a Comment