Friday, July 27, 2012

Jk azindua karakana ya ndege mali ya shirika la ndege la Precision air.

 Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi shirika la ndege la precision air Michael Shirima, akimpa zawadi Rais Jakaya Kikwete mara baada ya kuzindua karakana ya shirika hilo katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa JK Nyerere leo.

                                   Hapa akiwasili katika uzinduzi, anateta na watu wazima wenzie.

 Hapa anatoa hotuba na kuwashukuru Precision air kupiga hatua maana karakana hiyo itatumika pia na mashirika mingine ya ndege kwa maelewano. Kadhalika itatumika na wanafunzi wanaosomea kutengeneza na kurusha ndege.

 Hapa akitembezwa ndani ya karakana huku akiuliza maswali mawili matatu kama kawaida yake. lakini mkurugenzi mtenda wa shirika hilo Alfonce Kioko hakuwa mbali kuyajibu.

Mmoja wa mafundi wa shirika hilo akionyesha namna gani hawataki mchezo wanaposema wanazindua karakana. hakuna sualala maneno matupu bali kazi kwanza.

Chanzo: Blogu ya Full Shangwe.

No comments:

Post a Comment