Rais wa Uganda Yoweri Museveni amewataka watu kuepuka
kugusana moja kwa moja baada ya virusi hatari vya Ebola kuenea katika mji mkuu Kampala .
Watu kumi na wanne wamekufa
akiwemo mmoja mjini Kampala , tangu kuzuka kwa
ugonjwa huo magharibi mwa Uganda
wiki tatu zilizopita, alisema katika taarifa maalum kwa Taifa.
Ebola ni moja ya magonjwa hatari duniani.
Unaenea
kwa kugusana na unaua mpaka 90% ya watu walioambukizwa.
Bw
Museveni alisema maafisa wa afya wanajaribu kufuatilia kila mmoja ambaye ana waathirika
ili kwamba waweze kuwekewa Karantini.
Watu
hawana budi kuepuka kuepeana mikono, kubusiana au kufanya mapenzi kuzuia kuenea
kwa ugonjwa huo, aliongeza.
Bw
Museveni alisema ndugu na amrafiki wasimzike mtu yeyote anayehisiwa kuwa
amekufa kwa Ebola.
"Badala
yake awaite wafanyakazi wa afya kwa sababu wanajua namna ya kufanya mazishi
hayo,” alisema.
Bw
Museveni alisema madaktari saba na wafanyakazi 13 katika hospitali ya Mulago
hospitali kuu ya rufaa mjini Kampala
– wako kwenye karantini “baada ya tukio la mtu mmoja au wawili” kupelekwa huko.
Mtu
mmoja aliyeathirika baadaye alikufa.
"Nawatakia
kheri, na Mungu azipumzishe kwa amani roho za wale waliokufa " Bw Museveni
alisema wakati akimaliza hotuba yake kwa Taifa.
Muathirika
wa kwanza wa ugonjwa huu alikuwa mama mjamzito katika wilaya ya Kibaale kiasi
cha kilometa 170(maili 100) magharibi mwa Kampala .
Baadaye
ukasambaa wakati wa mazishi, alisema Rais Museveni.
Uliokuwa
hatari kabisa ni wa mwaka 2000 wakati watu 425 waliambukizwa. Zaidi ya nusu yao walikufa.
Hakuna
chanjo ya virusi hivyo. Dalili zake ni kupata homa ya ghafla, udhaifu, kuumwa
kichwa kutapika na matatizo ya figo.
No comments:
Post a Comment