SERIKALI
imesema kuwa hakuna malipo ya kiasi kidogo cha fedha
kilicholipwa kwa waathirika wa mlipuko wa mabomu ya Kambi
ya jeshi ya Mbagala yaliyotokea mwaka 2009 kama
ilivyoripotiwa na gazeti moja la kila wiki la hapa nchini hivi karibuni.
Akizungumza
na Idara ya Habari( MAELEZO) jana ofisini kwake , Mkuu wa Mkoa wa Dar es
Salaam, Said Meck Sadick alisema hakuna fidia ya Shs. 1400 na Shs.
2500 iliyotolewa kuwa ni ya uharibifu wa jumla ya fidia za malipo kwa wahanga
hao, bali malipo hayo ni tofauti ya kiasi cha fedha
kilichokuwa kinadaiwa na wahanga hao ambacho kilichobakia.
‘’
Unajua malipo ya wahanga hao yalifanyika katika awamu
mbili. Hivyo kiasi cha fedha cha malipo hayo yaliyotolewa
katika hundi hizo , ambayo iliripotiwa katika gazeti hilo ni malipo ya awamu ya
tatu. Malipo hayo ni tofauti ya
fedha kilichokuwa kinadaiwa na si kweli kuwa wahanga hao
walilipwa fedha hizo kama jumla ya fidia za malipo yao,’’ alifafanua Mkuu huyo
wa Mkoa.
Mkuu
huyo wa Mkoa, aliongeza kuwa habari hiyo iliyoandikwa sio sahihi na
haikufuata maadili ya uandishi wa habari kwani hakuweka wazi usahihi wa taarifa
hiyo.Serikali haijamdhulumu mtu yeyote, bali inalipa kutokana malipo stahili.
‘’Ninaomba
waandishi wa habari waandike habari walizozifanyika utafiti wa kina wa pande
zote ilikuepusha utoaji wa taarifa zisizosahihi,’’ alisisitiza.
Aidha
Mkuu huyo alisema malipo ya waathirika hao yanatolewa kwa awamu tofauti na kwa
idadi ya watu maalum, kwa sababu ya kuepusha utoaji wa malipo yasiyostahili.
Hivyo aliwataka waathirika hao kuvuta subira kwa kuwa malipo hayo
bado yanaendelea.
Naye
Mtathimini Mkuu wa malipo hayo, Victor Ndonne akizungumzia kuhusu
suala hilo
alisema hundi za malipo ya sh. 1000 na zilizotajwa hapo juu ni za tofauti ya
kiasi cha fedha kilichobakia baada ya wahanga hao kutoridhika na
malipo hayo yaliyotolewa katika awamu ya kwanza na awamu ya pili.
‘’
Fedha hizi zimelipwa baada ya kufanyika kwa tathimini mpya Agosti 18 mwaka
2011, ambapo ilioneka baadhi ya wahanga hawakurithika na
fidia walizolipwa,’’ alisema Ndonne .
Alifafanua
kuwa orodha ya wahanga wanaodaii malipa yao ni 2,575, hivyo hundi
zilizotolewa hadi sasa ni 295 kwa ajili ya malipo hayo, ambapo hundi 244
zimeshakabidhiwa kwa wananchi husika, hundi nyingine 18 majina yamebandikwa
katika eneo la Mbagala Kuu na Ofisi ya Mkurugenzi wa Wilaya ya
Temeke, zaidi ya wiki moja iliyopita na wanasubiri wananchi waende kuchukua.
Ndonne
alisema hundi 32 zimeonekana kuwa na matatizo mbalimbali mfano
majina ya vitambulisho vyao ni tofauti na yaliyoandikwa katika hundi na majina
mengine ya hundi hizo wahusika wameshafariki dunia. Aidha aliongeza kuwa hundi
moja imeonekana majina yamejirudia.
Alisema
kuwa hundi za malipo ya fedha ya wahanga hao zilitolewa kabla ya
mwisho wa mwaka wa fedha uliopita. Malipo ya fedha zingine zitatolewa mwaka huu
wa fedha wa 2012/2013 mara baada ya Serikali kuidhinisha.
No comments:
Post a Comment