Huu ni mtaa wa matunda, upo nyuma ya kituo cha polisi Buguruni. Leo mchana huu.
Huu ni mtaa wa wahindi watupu Kisutu hii karibu na DTV. Hata aina ya bidhaa ziuzwazo ni za wahindi.
Hiki ni kipita shoto cha DTV, makutano ya barabara ya Jamhuri na Makunganya Dar es salaam leo mchana.
Picha hii itaingia katika orodha ya picha nilizozipiga kwa taabu sana. Huyu ni Jordan Balindo, sijaonana nae yapata mwaka sasa. Nilikuwa nae Kampala chuoni, lakini baadae akawa anafanya shughuli zake Kenya, tumekutana leo kwenye daladala tukitokea Posta tulizungumza mengi sana, nikahitaji picha yake iwe kumbukumbu.
Akaniambia anashuka Mwenge, na mimi nilikuwa ninashuka kituo cha Sayansi (vituo vitatu nyuma) nikaamua kuenda mpaka Mwenge ili niweze kuipata picha hii, baadae nikarudi kwa mguu mpaka bamaga na kuchukua bajaj kuelekea nyumbani Ali maua Tandale.
Bwana Jordan ameamua kuwa mwanamuziki wa nyimbo za injili, na hapa alikuwa anaelekea chuo kikuu cha Mlimani ili kurekodi video yake. Haya wadau subirini video ya injili.
Hii picha ni moja ya harakati zangu za kupinga ombaomba mjini. Tazama huyu baba anaharibu maisha ya binti yake. Badala ya kumpa urithi wa elimu kwa umri huu yeye anazunguka nae mitaani kuombaomba.
Unadhani huyu mzee amebakisha miaka mingapi kuiaga dunia, na huyu binti atakuwa na maisha ya namna gani bila elimu kwa wakati huu. Kikubwa ataolewa na kunyanyaswa na mijanaume isiyo na huruma, hatokuwa na pa kukimbilia isipokuwa kusubiri hatima yake chungu.
No comments:
Post a Comment