Wednesday, August 22, 2012

Miradi Bubu ya wazalendo....

Ndugu zangu,

Nilipokuwa kidato cha tano shule ya Sekondari MOA (Mwenge Open Academy), nilisoma kitabu kimoja kikitwa ‘Miradi bubu ya wazalendo’ kilichoandikwa na mwanafasihi maarufu Tanzania na mshairi wa siku nyingi Ndugu Gabriel Ruhumbika.

Kama ilivyo kawaida ya wanafunzi nilisoma kitabu kile bila ya kufuata mazingatio ya yaliyokuwamo ndani na malengo ya mwandishi kuwafikishia hadhira yake.

Sasa nimekuwa mpenzi mzuri wa vitabu, natamani kukitafuta kitabu kile lakini sijui nitakipata wapi, ila kama kawaida yangu nikikipata nitakipiga picha na kukiweka kwenye blogu yenu ili nanyi kama mtataka kukinunua mukione kinavyofanana.

Leo nilipotoka ofisini asubuhi baada ya kikao cha kujadili gazeti letu linalotoka kila jumatano niliamua kupitia kwa dada ili kupata mazungumzo mawili matatu na kugonga chai, niliamua kutembea kwa miguu ili niweze kujione Tandale ilivyo, maana nyumbani si mbali na alipo dada. Kama vituo vitatu hivi, ila uvivu unatufanya tunaabudu kupanda daladala ama bodaboda, leo nikaamua kuuvunja mnyororo wa uvivu.

Sikuondoka patupu, kila nilipopita nilikuta watu wanajituma kuanzisha miradi midogomidogo ambayo kimsingi huwaingizia chochote. Nikajiuliza swali moja, hivi miradi hii imesajiliwa ama kurasimishwa na taasisi za kiserikali kama ‘MKURABITA’ (Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za wanyonge Tanzania) ili kama watahitaji kusaidiwa ama kuomba mkopo katika kanzi ‘Bank’ waweze kupata bila matatizo? Ndipo nikakumbuka kile kitabu cha ‘Miradi bubu ya wazalendo’

Hebu nanyi itupieni jicho miradi hii na mtoe maoni yenu ikiwezekana…. Kumbuka miradi hii yote ipo sehemu moja kila baada ya hatua kumi unakutana na mradi mpya unaofanana na wa awali. Je wamepewa mafunzo ya ushindani wa kibiashara, tatizo lipo wapi kwa wafanyabiashara wenyewe ama viongozi wa Serikali za mitaa, vijiji na Serikali kuu kupitia wizara ya viwanda na biashara?

HAFIDH KIDO
DAR ES SALAAM, TANZANIA
0713 593894/ 0752 593894
22/08/2012
kidojembe@gmail.com

2 comments:

  1. Ndugu Kido,

    Awali ya yote naomba nikufahamishe furaha yangu kutambua wewe, ulikuwa mpenzi wa kusoma ni wajina wangu. Habari wajina...

    Jana majira ya saa tatu na nusu usiku nilihitimisha saari yangu ya kusafiri katika bahari ya simulizi ya Ndugu Ruhumbika katika kitabu chake cha "MIRADI BUBU YA WAZALENDO" nami leo nilikuwa ninashauku ya kutafuta kama mwandishi mwenyewe aliwahi kuandikia kitu kuhusu kitabu hicho hapa mtandaoni na ndipo nilipokutana na huu kurasa wako na makala yako.

    Nimefurahishwa sana na kitabu hiki lakini kuna maswali kadhaa wa kadhaa ninayo juu ya mwandishi na hadithi lakini... kwa kuwa nimeona namba yako basi si mbaya naweza kukushirikisha na hata kubadilishana mawazo kidogo.

    Jasper "Kido" - Rasmi Jasper, Almaarufu Kido

    ReplyDelete
  2. Ndugu Kido,