Tuesday, May 14, 2013

Angalia safari ya Chelsea kuelekea Uholanzi kupambana na Benfica fainali ya Uropa Ligi kesho.

 Juan Matta akichekelea wakati akipanda basi kuelekea uwanja wa ndege tayari kwa safari.

 Baadhi ya wachezaji wa Chelesea wakizungumza mawili matatu wakati wakijiandaa kuelekea uwanja wa ndege.

                                                         David Luiz akipozi kwa picha.

Vijana wa darajani wakiwa ndani ya basi kuelekea uwanja wa ndege wakitoka uwanja wa mazoezi wa Cobham.

Kocha mkuu wa Chelsea Rafael Benitez kesho atakiongoza kikosi cha wana darajani katika kusaka taji la Uropa Ligi kwa mara ya kwanza taangu kuanzishwa timu hiyo.

Chelsea itakuwa timu ya kwanza kuwa na vikombe viwili vya ulaya baada ya kuwa mabingwa watetezi katika kombe la klabu bingwa ulaya ambapo msimu huu walitolewa mapema katikla hatua ya makundi.

Benitez ambaye ni kocha wa muda wa Chelsea atachuana na Benfica kutoka Ureno katika uwanja wa Amsterdam Arena nchini Uholanzi kesho katika fainali hizo za soka zinazoheshimiwa barani ulaya.

KIDOJEMBE


No comments:

Post a Comment