Rais wa Kenya
Uhuru Kenyatta na ambaye anatuhumiwa na mahakama ya kimataifa ya makosa ya
jinai anatarajiwa kukutana na waziri mkuu wa Uingereza David Cameron ndania ya
siku tatu za ziara yake mjini London .
Makundi
ya haki za binadamu kutoka nchini Kenya yameishutumu ziara hiyo ya
Rais Kenyatta katika nchi za magharibi mapema tu baada ya kushidna katika
uchaguzi mkuu wan chi hiyo uliofanyika mwezi march mwaka huu.
Uingereza imesema itawasiliana na Rais Kenyatta baadhi ya mamabo ya msingi tu,akiwa katika ziara hiyo ambayo ni mwaliko wa mkutano kuhusiana na masuala ya mgogoro waSomalia
Uingereza imesema itawasiliana na Rais Kenyatta baadhi ya mamabo ya msingi tu,akiwa katika ziara hiyo ambayo ni mwaliko wa mkutano kuhusiana na masuala ya mgogoro wa
Tuhuma za mahakama ya kimataifa ya makosa ya
jinai ICC dhidi ya Rais Kenyatta ni kufuatia vurugu zilizotokea katika uchaguzi
wa mwaka 2007 ambapo inakadiriwa kuwa takriban watu 1000 waliuawa.
Kiongozi
huyo wa Kenya
amepangiwa kufika katika mahakama ya ICC huko The Hague mwezi Julai ili kuanza
kusikilizwa kwa kesi yake.
Bwana
Kenyatta alimshinda aliyelkuwa Waziri Mkuu wa Kenya Bwana Raila Odinga kwa
kupata asilimia 50.07 ya kura ikilinganishwa na asilimia 43.28% za mpinzani
wake mkuu.
Katika
taarifa kwa waandishi wa habari, offisi ya rais imesema kuwa Bwana Kenyatta
amewasili mjini London
jumatatu asubuhi.
"Wakati
wa ziara yake Rais Kenyatta atahudhuria mkutano wa Londo kuhusu Somalia na pia atafanya mazungumzo na Waziri
Mkuu wa Uingereza David Cameron kuhusu uhusiano kati ya Kenya na
Uingereza".
Afisa
mkuu wa shirika la Kenya la International Center for Policy and Conflict ,
Bwana Ndung'u Wainaina, amesema mualiko wa Bwana Uhuru Kenyatta "ni
usaliti kwa ajenda ya mkutano wa Somalia" ambapo una lengo la kumaliza
ukosefu wa usalama na ukiukaji wa sheria.
BBC SWAHILI
No comments:
Post a Comment