Kocha wa Everton David Moyes ambaye msimu ujao
atakuwa kocha mkuu wa Manchester United, amesema hakupanga kuondoka Goodison Park ila ilikuwa vigumu kukataa ofa ya
kuifundisha United.
Moyes mwenye umri wa miaka 50 ameyasema hayo wakati
akizungumzia mchezo wa siku ya jumapili wa ligi kuu soka nchini England .
Kauli hiyo ameitoa siku moja baada ya
kutangaza rasmi ataicha Everton mwishoni mwa msimu huu na kujiunga Manchester
United kama mrithi wa Sir Alex Ferguson ambaye
alitangaza kustaafu kufundisha soka baada ya msimu huu kumalizika.
Kocha
huyo raia wa Scotland
amesema kuwa alipanga kuongeza muda wa kuifundisha Everton baada ya kukaa kwa
miaka 11, lakini alipopewa mkataba wa miaka sita wa kuifundisha Manchester
United alishindwa kukataa.
"Sikupanga
kuondoka Everton, ila kiukweli ilipokuja ofa ya United, sikuweza kusema
hapana" Alisema Moyes ambaye alianza kucheza soka kwenye klabu ya Celtic.
Aidha
Moyes ambaye aligoma kujibu chochote kuhusu United, alisema anatambua
changamoto atakazokutana nazo hapo jumapili wakati atakapokuwa akiongoza timu
yake ya Everton katika mchezo wa ligi kuu England dhidi ya West Ham
Kocha
wa Celti, Neil Lennon amepinga uvumi wa kuwa huenda akamrithi Moyes kwenye
viunga vya Everton huku Michael Laudrup yeye akisema anataka kuendelea
kuifundisha Swansea .
BBC SWAHILI
No comments:
Post a Comment