Tuesday, May 14, 2013

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI






KATIBU Mkuu wa Chama chaDemokrasia na Maendeleo(CHADEMA), Mheshimiwa Wilbroad Slaa, leo, Jumatatu,Mei 13, 2013, amekaririwa na gazeti moja akidai kuwa Rais wa Jamhuri yaMuungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete na timu yake yakampeni, “ilikuwa ikisaka kura kwenye nyumba za ibada na kumwaga sumu mbaya ya udini ambayo sasa inaitesa Serikali nataifa” kwenye Kampeni za Uchaguzi Mkuu wa 2010.Aidha, katika habari hiyo iliyoandikwa chini ya kichwa cha habari,



“Dk.Slaa amlipua JK” kwenye gazeti linalounga mkono CHADEMA laTanzania Daima,MheshimiwaSlaa anadai kuwa migogoro yasasa ya kidini “inajengwa au kutengenezwa na Serikaliiliyojiki kusambaza sumu ya udini katika misikiti wakati wa kampeni za Urais mwaka 2010”.Kwa hakika, hakuna namna nyingine ama namna bora zaidi ya kuielezea kauli hii ya Mheshimiwa Slaa isipokuwa kwamba kauli hiyo ni riwaya nyingine isiyokuwa na mshiko. Ni uongo mtupu. Yake Mheshimiwa Slaa ni maneno
yasiyokuwa na ukweli wowote.Ni uzushi na santuri ambayo imezoeleka sasa kwa wananchi.

Kauli ya Mheshimiwa Slaa ni mwendelezo wa mtiririko usiokuwa na mwisho wa
ghiriba ambazo kamwe hazitafanikiwa za Mheshimiwa Slaa kuwahadaa wananchi
kuhusu ukweli wa mambo ulivyo katika nchi yetu. Rais Jakaya Mrisho Kikwete na
timu yake ya kampeni kwawakufanya kampeni za Uchaguzi Mkuu wa 2010, ama wa mwaka mwingine wowote, katika nyumba yoyote ya ibada iwe  msikitini ama kanisani ama
hekaluni ama nyumba nyingine yoyote ya ibada mahali popote katika nchi yetu.
Mheshimiwa Rais Kikwete hajawahi hata kufikiria kuchanganya dini na siasa.
Hana sababu ya kufanya hivyo. Anaelewa fika madhara ya udini kwa mustakabali wa nchi yetu, kwa umoja wa taifa letu na kwa mshikamno wa wananchi wake. Yoyote anayejaribu kumbebesha Rais Kikwete msalaba wa udini ana lake jambo na ni vyema atuambie fika Rais alitumia Msikiti upi, ama Kanisa lipi, mahali gani na kwa nyakati gani kufanya kampeni.
Vinginevyo, kauli ya Mheshimiwa Slaa itabakia ni kauli tu inayostahili kupuuzwa na wananchi,itabakia ni kauli ya mtu mzima anayetapatapa nakufanya jitihada kubwa
kujivunjia mwenye heshimakwa kutunga na kusambazauongo.
Tunanapenda kumshauriMheshimiwa Slaa kuwa kamahana jambo la maana la
kuwaambia wananchi ama ameishiwa na hoja ni vyema anyamaze, awaachie wananchi waendelee nashughuli zao za maendeleo,kuliko kuendeleza riwaya zake zisizokuwa na mshiko.Yake ni santuri iliyowachosha wananchi.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya
Rais,
IkuluDar es Salaam.
13 Mei, 2013
THE UNITED REPUBLIC OF
TANZANIA
DIRECTORATE OF
PRESIDENTIAL
COMMUNICATIONS
Telephone: 255-22-2114512,
2116898
E-mail:
ikulumawasiliano@yahoo.com
press@ikulu.go.tz
Fax: 255-22-2113425
 PRESIDENT'S OFFICE,
      THE STATE HOUSE,
              P.O. BOX 9120,
DAR ES SALAAM.
Tanzania.

No comments:

Post a Comment