Makachero wa FBI kutoka Marekani wamewasili nchini Tanzania
kusaidia katika upelelezi wa shambulizi la bomu lililotekelezwa katika kanisa
katoliki mjini Arusha siku ya jumapili.
Mwandishi wa BBC Baruan Muhuza akiwa mjini Arusha anasema
makachero hao wa FBI wako Tanzania
kusaidiana na Jeshi la wananchi wa Tanzania
na Polisi kutafuta undani wa tukio hili ambalo limeishtua na kuiweka serikali
ya Tanzania
katika wakati mgumu.
Baruan Muhuza anaongezea hali inaonekana kuwa
ngumu zaidi hasa kutokana na aina ya matukio ambayo yamekuwa yakitokea katika
siku za hivi karibuni yakihusisha viongozi wa dini ambapo wengi ya wanaodhurika
huwa ni wa imani ya kikristo.
Wakati
huo huo wakuu wa serikali wakishirikiana na viongozi wa kidini wameandaa
mkutano utakaojumuisha viongozi wapatao 200.
Mkuu
wa mkoa wa Dar es Salaam
Said Meck Sadiq amewaambia wanahabari kuwa wamelazimika kuandaa mkutano huo wa
siku mbili kufuatia agizo la Rais Jakaya Kikwete.
Mkutano
huo utajadili uhusiano bora baina ya wakrito na waislamu.
BBC SWAHILI
No comments:
Post a Comment