Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
limemtaka Shaffih Dauda ambaye ni mmiliki wa tovuti ya www.shaffihdauda.com kutoa maelezo kuhusiana na barua ya
Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) aliyoiweka kwenye mtandao wake
huo.
FIFA ambayo ilisimamisha mchakato wa uchaguzi wa
TFF baada ya baadhi ya wagombea kuulalamikia, baadaye ilitoa maelekezo kuhusu
mchakato huo kwa barua ambayo iliituma kwa Rais wa TFF, Leodegar Lenga.
Rais wa TFF katika mkutano wake na waandishi wa
habari ambao Dauda alihudhuria alibainisha kuwa barua hiyo ya FIFA hawezi
kupewa kila mtu, na kuruhusu waandishi kuisoma kwa Ofisa Habari wa TFF bila
kuondoka nayo.
Wakati Rais Tenga anazungumza na waandishi wa
habari (Mei 2 mwaka huu), nakala ya barua hiyo ya FIFA ilikuwa kwa viongozi
wakuu wa TFF pekee, na viongozi wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na
Michezo. Hivyo TFF imemtaka Dauda kutoa maelezo ya mahali alipoipata barua hiyo
ndani ya siku saba.
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa
Miguu Tanzania (TFF)
No comments:
Post a Comment