Tuesday, May 21, 2013

Safari ya mwisho ya mwasisi wa TANU, Mzee Ally Sykes.

 Rais Jakaya Mrisho Kikwet akiongoza mamia ya waombolezaji katika mazishi ya Mzee Ally Kleist Sykes, mmoja wa waasisi wa chama cha TANU, leo katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es salaam. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimfariji mjane wa marehemu Ally Sykes, Zainab Ally, wakati alipofika kuhani msiba huo wa mwasisi wa TANU, aliyefariki jana jijini Nairobi. Marehemu Sykes anazikwa leo jioni jijini Dar es Salaam

Makamu wa Rais akisalimiana na Waziri wa zamani Harith Mwapachu ambaye baba yake alikuwa miongoni mwa wapigania uhuru wa Tanzania, hapa ni nyumbani kwa marehemu Mzee Ally Sykes.

No comments:

Post a Comment