Mchezaji mkongwe wa Manchester United Rio Ferdinand
ametia saini mkataba wa mwaka mmoja hivyo kusalia katika klabu hiyo kwa
mwaka mmoja zaidi.
Shughuli hiyo iliyoidhinishwa na Meneja mpya
David Moyes - imehitimisha wasiwasi ulikokuwepo kuhusu uwezekano wa
mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 34 kutundika viatu vyake.
Ferdinand amesema: "nimefurahi. Imekuwa ni safari ya kufurahisha sana na natumai itaendelea kuwa hivyo."
Wakati akitangaza kuondoka kwake kama meneja wa Manchester United,Sir Alex Ferguson alisema Ferdinand amekuwa na wakati mzuri sana katika klabu hiyo na ataongezewa kandarasi.
Katika msimu uliomalizika mchezaji huo wa safu ya nyuma ameichezea Mashetani wekundu mara 34 kati ya mwaka 2012-13, hii ikijumuisha mechi 28 katika mechi za Ligi kuu ya Uingereza.
Ferdinand amesema : "nani hataki kukichezea klabu hiki tena mbele ya mashabiki 76,000 kila wiki?
"sasa naweza kujikita zaidi katika klabu yangu ambayo imeniweka vyema sana katika ile miaka ambayo nimekichezea.
Mchango wa Ferdinand katika timu ya Manchester United kulimfanya wakati mmoja kuchaguliwa na wenzake kuwa mchezaji bora zaid.
Mchezaji huyo wa zamani wa West Ham United na Leeds United ameichezea timu ya taifa ya Uingereza mara ,81 na alijiunga na Manchester United Julai 2002 kwa karibu £30m hivyo kuwa mchezaji wa ulinzi anayelipwa pesa nyingi zaidi duniani.
Kijumla Rio Ferdinand ameichezea Manchester United mara 432 na kushinda kombe la klabu bingwa bara ulaya mara moja na taji sita za ligi kuu ya Uingereza.
BBC SWAHILI
No comments:
Post a Comment