Upangaji ratiba (draw) ya Ligi ya Mabingwa wa
Mikoa (RCL) uliokuwa ufanyike juzi (Mei 3 mwaka huu), sasa utafanyika Jumanne
(Mei 7 mwaka huu) na ligi hiyo itaanza Mei 12 mwaka huu kama ilivyopangwa.
Uamuzi huo umefanya na Kamati ya Mashindano ya
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) iliyokutana leo (Mei 5 mwaka huu)
kujadili maandalizi ya ligi hiyo, yakiwemo maombi ya baadhi ya mikoa ambayo
haijamaliza yao
kutaka RCL isogezwe mbele.
Kamati ya Mashindano chini ya Uenyekiti wa
Blassy Kiondo ambaye pia ni mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF ilipitia maombi
hayo na kuangalia athari ambazo zinaweza kujitokeza huko mbele iwapo RCL
itasogezwa mbele.
Baadhi ya athari iwapo RCL itasogezwa mbele ni
timu zitakazopanda daraja kucheza Ligi Daraja la Kwanza (FDL) kutopata muda wa
kufanya usajili wa wachezaji kwa msimu mpya.
Hivyo draw hiyo itakayofanyika saa 6 mchana
itahusisha mikoa ambayo tayari imemaliza ligi na kuwasilisha majina ya mabingwa
wao. Mabingwa ambao wamewasilishwa na mikoa yao kwenye mabano ni Abajalo SC
(Dar es Salaam 2), Biharamulo FC (Kagera), Flamingo SC (Arusha), Friends
Rangers (Dar es Salaam 3), Katavi Warriors (Katavi), Kiluvya United (Pwani),
Kimondo FC (Mbeya) na Machava FC (Kilimanjaro).
Mingine ni Magic Pressure FC (Singida), Mbinga
United (Ruvuma), Mji Njombe (Njombe), Polisi Jamii Bunda FC (Mara), Red Coast
FC (Dar es Salaam 1), Rukwa United (Rukwa), Saigon FC (Kigoma), TECKFOLT FC ya
Kilombero ambayo ni Shule ya Sekondari (Morogoro) na UDC FC ya Ukerewe (Mwanza).
Mikoa iliyoshindwa kuwasilisha mabingwa wake ni Dodoma , Geita, Iringa,
Lindi, Manyara, Mtwara, Shinyanga, Simiyu, Tabora na Tanga.
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa
Miguu Tanzania (TFF)
No comments:
Post a Comment