London, England
Hatimaye kocha wa
Manchester City, Roberto Mancini ametimuliwa rasmi kuinoa timu hiyo baada ya
kukanusha uvumi huo mwishoni mwa wiki hii.
Uongozi wa Man City
umetoa taarifa yake Jumatatu na kuweka wazi kuwa “ameshindwa kutimiza malengo
ya klabu, kwa matarajio ya kuchukua ubingwa wa klabu bingwa Ulaya msimu ujao.”
Kocha msaidizi Brian
Kidd atasimamia mechi mbili zilizobaki za ligi kuu ya Uingereza na ziara yao ya
Marekani mwishoni mwa mwezi huu. Taarifa zinaeleza kuwa kocha wa Malaga, Manuel
Pellegrini kutoka Chile ndiye anayetajwa kuchukua mikoba ya Mancini kwa msimu
ujao.
Katika taarifa ya
kumtimua kocha huyo iliyosomwa na mwenyekiti wa klabu hiyo Khaldoon Al Mubarak,
inamshukuru kocha huyo mwenye miaka 48 ambaye ameanza kuinoa timu hiyo tangu
mwaka 2009 na kufanikiwa kunyakua ubingwa wa ligi hiyo mwaka 2012 ambapo Man
city kwa mara ya mwisho kuhukua ubingwa huo ni miaka 44 iliyopita.
Mbali ya ubingwa wa
ligi kuu pia Mancini amefanikiwa kunyakua ubingwa wa FA mwaka 2011 na kuifanya
kuwa ni timu yenye mafanikio sana tangu kujiunga kwake mwaka 2009.
“Rekodi ya Roberto
inazungumza yenyewe, ameweza kulinda mapenzi na heshima ya mashabiki wa Man
City, amefanya alichotuahidi na ameleta mafanikio. Ni maamuzi magumu sana
kutengana na Mancini lakini ni matokeo ya mipango na mapitio ya msimu huu kuwa
mabaya,” alieleza mwenyekiti Khaldoon.
HAFIDH KIDO
May 14, 2013
No comments:
Post a Comment