MWENYEKITI wa Umoja wa Wafanyabishara
Walemavu Dares Salaam (UWAWADA), Mohamed Kidumke amesema kama
serikali haitawasaidia mikopo walemvu basi kuna hatari baadhi ya watu hao
wakaendelea kuwa ombaomba barabarani milele.
Wakizungumza na wandishi wa habari
jijini Dar es Salaam juzi, Kidumke alisema badhi ya walemavu hao hawapendi
kukaa barabarani na kuomba bali wamekuwa wakifanya hivyo kutokana na kukosa
njia za kujiingizia kipato.
Alisema Umoja wao unania ya
kuwaondoa walemavu wote wanaomba barabarani kwa kuwaanzishia biashara
ndogondogo lakini bado jitihada zao hizo zinahitaji uungwaji mkono na serikali
kwa kuwapatia mikopo nafuu walemavu hao ili waweze kujikwamua.
“Wapatiwe mikopo pia watengewe
maeneo ambayo yatawezesha kukutana na wateja kwa wingi kwa mfano maeneo
wanayolenga ni kama vile kwenye vituo vya
daladala”alisema Kidumke.
Kidumke alisema ni muda mrefu umoja
huo uliuomba uongozi wa Halmashauri ya wilaya ya Ilala kuwatengea maeneo ya
kufanyia biashara lakini hadi sasa uongozi huo haujatoa jibu.
Alisema wakati mwingine viongozi
hao wamekuwa wakichukuliwa na umoja huo kama chanzo kimojawapo kinachokwamisha
juhudi za maendeleo yao
kwa kutozipatia ufumbuzi changamoto zinazowakabili.
Chanzo:www.fullshangweblog.com
No comments:
Post a Comment