CHAMA cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA),
kimezipongeza timu zake tatu zilizofuzu kucheza Ligi ya Mabingwa, baada ya
kumalizika kwa Ligi Daraja la Pili hatua ya sita bora Aprili 27 mwaka huu.
Timu hizo ni Red
Coast , Abajalo na Friends Rangers,
zitakazoungana na timu za mikoa mingine kucheza Ligi ya Mabingwa itakayoanza
Mei 12 mwaka huu chini ya Usimamizi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).
Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa DRFA, Mohamed
Mharizo, alisema ligi hiyo ilikuwa na ushindani wa hali ya juu na kuzitaka timu
zilizofuzu hatua hiyo kujipanga vizuri ili kuuwakilisha vyema mkoa na hatimaye
kucheza Ligi Daraja la Kwanza .
“Kwa niaba ya DRFA napenda kuchukua nafasi hii
kuzipongeza timu hizo kwa kufanya vizuri na kupata nafasi ya kuuwakilisha mkoa
wa Dar es Salaam katika kutafuta kucheza Ligi
Daraja la Kwanza msimu ujao wa 2013/2014.
“Tunaamini watajiandaa vyema na kutuwakilisha
vizuri katika ligi hiyo, kufanya kwao vizuri ndio itakuwa fahari yetu DRFA na
wadau wa mpira wa miguu mkoa wa Dar es
Salaam , tunawatakia kila la kheri na tupo pamoja
katika kushirikiana nao.
Ligi Daraja la Pili hatua ya sita bora mkoa wa Dar es Salaam ilianza
Aprili 15 mwaka huu ambapo ameziomba timu za Sharif Stars, Day Break na Boom FC
zilizoshiriki ligi hiyo kujiandaa vizuri kwa ajili ya mashindano yajayo.
No comments:
Post a Comment