KUSIMAMISHWA KWA
MAFUNZO YA SHAHADA ZA UZAMILI NA UZAMIVU
Kufuatia
kuendesha mafunzo ya shahada ya Uzamili (Masters) na Shahada za Uzamivu (PhD)
kinyume cha utaratibu na kutokua na wahadhiri wa kutosha wenye sifa stahili,
Tume katika mkutano wake wa hivi karibuni ulikiamuru Kampala International
University , Kampasiya
Dar-es-Salaam ifuatayo;
- KIU isimamishe mara moja
mafunzo yote ya shahada za juu (Postgraduate) ikiwa ni pamoja na Shahada
za Uzamili (Masters) na Shahada za Uzamivu (PhD) katika kampasi ya
Dar-es-Salaam
- KIU ishirikiane na
wanafunzi wote iliyowadahili katika program zilizotajwa hapo juu
wawezekuhamia kwenye vyuo vingine vyenye idhibati ya kutoa mafunzo hayo.
Tume haitatambua
shahada yeyote ya Uzamiili au Uzamivu itakayotolewa na chuo hicho kwa
watakaosoma katika kampasi ya Dar-es-Salaam.
Angalizo:
Chuo cha KIU
Kampasi ya Dar-es-Salaam kina ithibati na kitaendelea kutoa mafunzo ya shahada
ya kwanza (Bachelors), Diploma au vyeti zilizopitishwa na TCU kwa mujibu wa
Ithibati husika tu.
Imetolewa na:
Katibu Mtendaji
TUME YAVYUO VIKUU
TANZANIA
(TCU)
No comments:
Post a Comment