Polisi nchini Kenya wamekabiliana na waandamanaji
waliozingira majengo ya bunge kulaani jaribio la wabunge kutaka kujiongeza
mishahara.
Polisi hao wametumia gesi ya kutoa machozi pamoja na maji
kuwatawanya waandamanaji hao ambao wengi wao ni wanachama wa mashirika ya
kijamii ambao wamesema katu hawaondoki katika majengo hayo ya bunge hadi wabunge
watakapopata ujumbe wao.
Pia inaarifiwa kuwa wanawataka wabunge kutia
saini na kuapa kuwa hawatatumia bunge kunyanyasa wananchi maskini kwa
kujiongeza mishahara kinyume na sheria.
Mashirika
ya kijamii yaliandaa maandamano hayo kuonyesha ghadhabu waliyonayo wakenya
dhidi ya wabunge hao wanaotaka kuongezwa miashara, miezi miwili tu baada ya
kufanyiika uchaguzi mkuu wa amani.
Aidha
waandamanaji hao walipeleka Nguruwe kwenye mlango mkuu wa kuingia katika bunge
pamoja na damu kama ishara kuwa wabunge ni
watu walafi na wasiojali maslahi ya wakenya kwa kujitakia makubwa.
Maandamano
haya yanakuja siku moja baada ya tume ya kitaifa ya mishahara ambayo wajibu
wake ni kudhibiti mishahara ya wafanyakazi wa umma kusema kuwa katu
haitawaongeza mishahara wabunge.
Tume
hiyo ilisema siku ya Jumatatu kuwa haitaogopa vitisho vya wabunge kutaka
kuivunjilia mbali tume hiyo ikiwa hawatawaongeza mishahara wabunge kama kikwazo.
Wabunge
hao walijaribu kwa kutumia vitisho kuilazimisha tume hiyo kuwoangeza mishahara
lakini hawakufua dafu.
Ni
baada ya mbunge mmoja kuwasilisha hoja bungeni kuwa ikiwa tume hiyo
haitawaongeza mishahara watafanyya kila hali kuivunja.
Hata
hivyo tume hiyo ni ya kikatiba.
Wabunge
wa Kenya
wanataka kulipwa mshahara wa shilingi 850,000 wakati wakihudumu katika bunge la
kumi ikipuuza mshahara waliowekewa na tume ya mishahara ambao ni shilingi
532,000. Wanasema pesa hizi ni kidogo sana .
BBC
SWAHILI
No comments:
Post a Comment