Rais Andry Rajoelina wa Madagascar
amesajili jina lake
kugombea Urais katika
uchaguzi mkuu wa mwezi wa Julai licha ya kusema kwamba hangegombea.
Jina lake
limejitokeza katika
orodha ya wagombea 41 wa Urais waliopitishwa na tume ya uchaguzi .
Bw Rajoelina, akiungwa mkono na jeshi
,alimgo'wa madarakani Marc Ravalomanana mnamo mwaka 2009,na kukitumbukiza
kisiwa hicho katika machafuko ya kisiasa.
Baada
ya chagizo kutoka nchi za kanda viongozi wote wawili walikubaliana kutogombea
uchaguzi wa mwezi wa Julai.
Lakini
mshauri maalum wa Bw Rajoelina amesema makubaliano hayo yalivunjwa pale mke wa
Bw Ravalomanana , Lalao, kuamua kugombea.
"sasa
mchuano uko wazi kwa kila mtu," Augustin Andriamananoro ameliambia shirika
la habri la Reuters.
Mama
Ravalomanana aliejea nchini mwezi Machi kutoka Afrika ya Kusini,ambako yeye na
mume wake walikimbilia baada ya kungo'lewa madarakani.
Maafisa
wa serikali nchini Madagascar
wamezuia juhudi kadhaa za Bw Ravalomanana kurejea nchini,wakitaja kua na khofu
za kuzuka machafuko.
Aliyekua
Rais Didier Ratsiraka, mwenye umri wa miaka 76, ambae alikwenda uhamishoni kwa
miaka kadhaa baada ya kushindwa na Bw Ravalomanana katika uchaguzi uliozusha
ubishi mkali mnamo mwaka 2002, nae pia yumo katika orodha ya wagombea.
Bwana
Rajoelina alipata umaarufu kama dj kabla ya
kuingia katika siasa.
Mapinduzi
ya 2009 yaliiacha Madagascar
ikipigwa pande na jamii ya kimataifa na kunyimwa misaada na mataifa ya kigeni.
BBC SWAHILI
No comments:
Post a Comment