Mcheza filamu mashuhuri sana duniani,Angelina Jolie
amesema kwamba amekatwa matiti yake yote pamoja na kuondoa mfuko wake wa uzazi.
Kwenye taarifa aliyoandika kwenye gazeti la New York Times,
Bi Jolie amesema alifanyiwa uchunguzi wa celi zake na kugunduliwa kwamba
alikuwa katika hatari kubwa sana
ya kupata saratani ya matiti. Ndipo akaamua kukatwa matiti yake mawili.
Angelina mwenye umri wa miaka 37 na mama na
watoto sita, alipoteza mamake mzazi kutokana na maradhi ya saratani ya matiti.
Anasema
aliandika taarifa hiyo kuwahakikishia watoto wake kwamba hakuwa kwenye hatari
ya kupata saratani tena.
Kulingana
na Jolie madaktari walisema kuwa uwezekano wake kupata Saratani ya matiti ni
asilimia 87 huku akiwa na asilimia 50 uwezo wake wa kuugua Sarati ya mfuko wa
uzazi.
''Niliamua
kuchukua hatua mwenyewe ili kuzuia uwezekano wowote wa kuugua Saratani hiyo,''
alisema Jolie.
Alisema
kuwa shughuli hii ilianza mwezi Februari na kukamilika mwishoni mwa mwezi
April.
Uwezekano
wapunguzwa.
Katika
taarifa iliyoandikwa na Bi Jolie na yenye kichwa, 'Uamuzi wangu wa kimatibabu',
Bi Jolie alieleza kuwa mamake alipambana na Saratani kwa miaka kumi na kufariki
akiwa na umri wa miaka 56.
Alisema
kuwa alielewa fika kuwa siku moja atawahi kuugua Saratani na ndio maana
akachukua uamuzi wa kufanyiwa upasuaji huo mgumu wa wiki tisa ambao ulihitaji
kukatwa matiti.
Uwezekano
wake wa kuugua saratani sasa umeshuka kutoka 87% hadi 5%.
Alimsifu
mumewe Brad Pitt, kwa kumuunga mkono na kumfariji kwa kila aliyopitia, na
kusema kuwa ametulizwa na kuwa wanawe hawakupata lolote katika matokeo ya
uchunguzi wa madaktari tangu kufanyiwa upasuaji.
"ninahisi
kuwa na nguvu kwa uamuzi niliofanya, na kwa kuwa ninasalia kuwa mwanamke hata
baada ya kuondoa viungo hivyo,'' alisema Bi Jolie.
"kwa
mwanamke yeyote anayesoma maneno haya, natumai ataweza kujua kuwa wanaweza
kufanya uamuzi.''
Muigizaji
huyo, ambaye ameshinda tuzo nyingi kwa uigizaji wake, pia ni mtunzi wa filamu
na mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa anayehusika na harakati za kibinadamu.
Wakati
alipokuwa anafanyiwa upasuaji, Bi Jolie alizuru Jamuhuri ya Kidremokrasia ya Congo pamoja na
waziri wa mambo ya nje wa Uingereza William Hague.
Jolie
pia alihudhuria mkutano wa mawaziri wa mambo ya nchi za kigeni wa G8,
kuhamasisha dunia kuhusu dhulma za kingono katika maeneo ya vita.
BBC SWAHILI
No comments:
Post a Comment