Monday, May 13, 2013

Wagonjwa wa akili wapatao 40 watoroka hospitali ya Mathare nchini Kenya.


Polisi wanawatafuta wagonjwa karibia arobaini waliotoroka kutoka hospitali ya watu wenye matatizo ya kiakili, mjini Nairobi ya Mathare. Wagonjwa hao wanasemekana waliwashinda nguvu walinzi wao na kutoroka.
Zogo hilo lilizuka katika hospitali ya Mathare baada ya kutokea hali ya sintofahamu iliyowahusisha wafungwa arobaini wanaume.
Baadhi ya vyombo vya habari vinasema kuwa wagonjwa hao walikuwa wanalalamikia hali mbaya na kibinadamu katika hospitali hiyo.

Taarifa zaidi zitaujia baadaye katika blogu yako ya kijamii.

HAFIDH KIDO

No comments:

Post a Comment