Waziri wa Ulinzi wa Libya , Mohammed al –Barghathi
amejiuzulu wadhifa wake huo akipinga kushikiliwa kwa majengo ya wizara za
sheria na mambo ya nje na wanamgambo wenye silaha.
Wanamgambo hao wamekuwa wakidai kupitishwa kwa
sheria inayowapiga marufuku maafisa wa serikali ya kiongozi wa zamani wan chi
hiyo hayati Kanali Muammar Gaddafi, kupewa nyadhifa za kisiasa.
Jumapili
iliyopita, ikiwa ni moja tangu wanamgambo hao wayashikilie majengo, bunge
lilipitisha sheria hiyo.
“Sitakubali
kwamba, siasa zitaendeshwa kwa nguvu ya mtutu wa bunduki,” shirika la habari la
Reuters limemkariri waziri huyo wa ulinzi akisema.
Wanamgambo
hao walidai kwamba, hawataondoka katika majengo hayo kabla ya kupitishwa kwa
sheria hiyo inayowapiga marufuku maafisa hao wa zamani waliokuwa na nyadhifa
wakati wa serikali ya Kanali Gaddafi.
“Hii
ni sawa na kuishambulia demokrasia niliyoapa kuilinda,” amesema Bw. Barghathi
amabye aliwahi kuwa kamanda wa jeshi la anga huko Benghazi kabla ya kustaafu na kulipwa mafao
ya serikali mwaka 1994.
kutengwa
kisiasa
Mwandishi
wa BBC mjini Tripoli ,
Rana Jawad, anaripoti kuwa Sheria ya Kuwatenga kisiasa pia itamhusu Bw.
Barghathi wakati itakapoanza kutumika.
Inaonekana
amejiuzulu kabla ya kufukuzwa. Sheria hiyo huenda ikawaathiri maafisa wengine
waandamizi wa serikali akiwemo Mkuu wa Baraza la taifa la Congress, Mohammed al
– Megaryef.
Alijitoa
kutoka serikali ya Kanali Gaddafi miaka ya themanini baada ya kuhudumu kama
balozi wa Libya nchini India .
Mwandishi
wetu anasema, tangu sheria hiyo ipitishwe wanamgambo kadhaa wameondoka kutoka
majengo hayo, lakini baadhi ya vikundi vya wapiganaji wenye silaha nzito vimebakia.
Wale wanaoshikilia jengo la wizara ya nje,
ambalo lilikuwa la kwanza kulengwa Jumapili ya Aprili 28 wamesema wako tayari
kuondoka lakini bado hawajaondoka.
Nao
wanamgambo nje ya wizara ya sheria iliyoxingirwa Jumanne iliyopita wamesema
wanasubiri maafisa wa ulinzi wa serikali kuchukua nafasi yao .
Baraza
la Juu la Mapinduzi ambacho ni chombo kinachodai kuwawakilisha wapiganaji
kadhaa wa zamani na kinachoaminika kudhibiti baadhi ya makundi yenye silaha,
limeiambia BBC kwamba, linataka Waziri Mkuu, Ali Zidan aondolewe madarakani.
Mwandishi
wetu anaripoti kuwa, Waziri Mkuu ambaye inasemekana hataguswa na sheria hiyo
mpya, hivi karibuni alivielezea vikundi vyenye silaha kama
watu walioshindwa katika uchaguzi uliofanyika nchi nzima mwaka jana.
Kanali
Gaddafi aliondolewa madarakani na hatimaye kuuawa wakati wa vuguvugu la mageuzi
mwaka 2011 baada ya kuitawala Libya
kwa zaidi ya miaka 40.
BBC SWAHILI
No comments:
Post a Comment