Tuesday, May 14, 2013

Xavi ampiku kocha wake wa zamani kwa kutwaa mataji ya La Liga Barcelona.


Mchezaji wa Barcelona Xavi Hernandez amevunja rekodi ya kocha wake wa zamani Pep Guardiola, kwa kutwaa taji la ligi kuu ya Hispania La Liga mara saba tangu alipoanza kuichezea timu hiyo mwaka 1998.

Kwa mujibu wa taarifa za timu hiyo Xavi alianza kuichezea timu hiyo akiwa msaidizi wa Pep Guardiola ambaye alishatangaza kuachana na timu hiyo ili kuenda kumalizia soka lake katika nchi nyingine kwa lengo la kupata uzoefu wa ligi mbalimbali kwani alikuwa na malengo ya  kugeukia ukocha.

Guardiola anayekinoa kilabu cha Bayern Munich, ndiye aliyekuwa mchezaji anayeongoza Barcelona kwa kutwaa mataji mengi ambapo alitwaa mataji sita tangu alipojiunga na kikosi hicho mwaka 1990 mpaka alipoagana na kikosi hicho mwaka 2001, ambapo alikwenda vilabu vingine vya Brescia, Roma, Al Ahli ya Qatar na kumalizia kucheza soka mwaka 2006 katika kilabu cha Dorados nchini Mexico.

Baada kusomea ukocha timu ya kwanza kujiunga nayo ni Barcelona B mwaka 2007 kabla ya kutwaa rasmi mikoba ya aliyekuwa kocha wa Barcelona, Frank Rijkaard mwaka 2008 mpaka 2012 alipoaga rasmi na kujiunga na Buyern Munich ambapo ataanza rasmi kazi yake mwezi Julai mwaka huu.

Aidha miaka ambayo Xavi Hernandez alichukua ubingwa wa La Liga akiwa na Barcelona ni mwaka 1999, 2005, 2006, 2009, 2010, 2011 na 2013.

Kwa upande wa Pep Guardiola amenyanyua kikombe cha La Liga akiwa na FC Barcelona katika msimu wa mwaka 1991, 1992, 1993, 1994, 1998 na 1999.

HAFIDH KIDO
14 May, 2013
DAR ES SALAAM, TANZANIA
<

No comments:

Post a Comment