Maafisa wa Uchina wameanzisha uchunguzi juu ya afisa wa
ngazi ya juu katika kile kinachoonekana kama
hatua ya hivi karibuni ya kiongozi wa nchi hiyo Xi Jinping ya kukabiliana na
ufisadi.
Katika ripoti fupi iliyotolewa na serikali ya Uchina kupitia
shirika la habari la uchina Xinhua imesema kuwa Liu Tienan - mkuu wa sera za
uchumi - alisimamishwa kazi baada ya kushutumiwa kukiuka vikali nidhamu.
Hii ni kesi ya kwanza kwa afisa wa ngazi ya
juu wa uchina kutolewa hadharani tangu mwaka jana baada ya mwandishi wa habari
wa kichina kumshutumu wazi Bwana Liu kwa ufisadi , kugushi vyetii vyake vya
elimu na kutishia kumuua hawara wake .
Nchini
Uchina ambako vyombo vya habari vinabanwa , shutuma hizi ni kubwa dhidi ya
afisa wa ngazi ya juu. Lakini sasa maafisa wanasema bwana Liu anachunguzwa ,
licha ya kwamba hawakueleza bayana anakabiliwa na shutuma gani hasa .
Tangu
aingie mamlakani Rais Xi Jinping - aliapa kukabiliana na ufisadi , akionya kuwa
ni tisho kwa utawala wa chama chake cha kikomunisti .
Uchunguzi
huu utaangaliwa kama jaribio kwa rais mpya la
kuweza kushawishi umma kuwa anaweza kweli kumaliza uhalifu huo.
BBC SWAHILI
No comments:
Post a Comment