Saturday, May 11, 2013

MTEKAJI WA OHIO ALIZAA NA MATEKA.


Ariel Castro akiwa mahakamaniMamlaka ya Marekani imesema ushahidi wa vipimo vya DNA umethibitsha kuwa Ariel Castro mtuhumiwa wa utekaji wa wanawake watatu kwenye nyumba moja mjini Cleveland,Ohio kwa zaidi ya miaka 10 ni baba wa mtoto wa miaka sita aliyekutwa kwenye nyumba hiyo.

Binti huyo Jocelyn mwenye miaka sita ni mtoto wa bi Amanda Berry ambaye aliokolewa pamoja na wanawake wengine siku ya jumatatu.
Polisi nchini Marekani wamesema kuwa ushahidi huo wa awali unaonyesha kuwa, mtoto huyo alizaliwa na Amanda wakati akiwa ametekwa kwenye nyumba hiyo na bwana Castro.
Wakati huo huo, mmoja wa wanawake waliokuwa wametekwa kwenye nyumba hiyo kwa zaidi ya miaka kumi, Michelle Knight ametoka hospitalini na kutoa taarifa za kusema anahitaji uhuru binafsi.
Michelle Knight ametoa taarifa ya kusema yupo katika hali nzuri na anahitaji uhuru binafsi huku ikishindwa kujulikana alipokwenda.
Taarifa za awali za polisi zilisema bi Michele aliteswa na kupigwa kwa siku tano za mwanzo baada ya kutekwa mwaka 2002 na bwana Castro.
Ariel Castro aifikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza alhamisi, ambapo mapema jumatatu wanawake watatu walipatikana kwenye nyumba yake baada ya kupotea kwa miaka zaidi ya kumi.
BBC SWAHILI

No comments:

Post a Comment