Tuesday, May 7, 2013

Mtoto wa Kitanzania ashinda mchezo wa karate nchini Marekani.


Mtoto Mwita Matinyi (pichani kushoto), Jumapili iliyopita alipata furaha kubwa baada ya kutwaa ushindi wa tatu kwenye Michuano ya Nne ya Kaizen Karate ya Kila Mwaka inayotumia mtindo wa Goju Ryu iliyofanyika kwenye Shule ya Kati ya Kimataifa ya Silver Spring jimboni Maryland, kilomita mbili nje ya Jiji la Washington DC. Kevin mwenye umri wa miaka tisa, alishinda kwenye michuano ya kupigana ulingoni kwa watoto wenye mkanda wa rangi ya machungwa. Mdogowe, Chacha Matinyi, mwenye umri wa miaka 6 (pichani kulia), ingawa hakuibuka na ushindi lakini alijitahidi na kuacha matumaini makubwa ya kushinda mwakani. Watoto hawa walikuwa Watanzania pekee walioshiriki michuano hiyo iliyofurika watoto wa rika mbalimbali ambayo majaji wake wenye vyeo cha Grand Masters walikuja kutoka California mahsusi kwa kazi hiyo. Watoto hawa wameyazima makeke ya baba yao, Mobhare Matinyi, ambaye alikuwa akiwaringishia medali zake alizopata enzi akiwa bondia wa light heavy weight chuo kikuu nchini India.
MJENGWA BLOG

No comments:

Post a Comment