Taifa Stars imepangwa kundi A la michuano ya
Kombe la COSAFA ambapo itacheza mechi yake ya kwanza Julai 6 mwaka huu jijini Lusaka , Zambia
dhidi ya Shelisheli.
Upangaji ratiba (draw) wa mashindano hayo
ulifanyika juzi (Mei 3 mwaka huu) jijini Lusaka
ambapo timu nyingine zilizo na Taifa Stars katika kundi hilo
ni Namibia na Mauritius .
Kundi la Taifa Stars litachezea mechi zake jijini Lusaka .
Mechi ya pili ya Taifa Stars katika hatua ya
makundi itakuwa Julai 8 mwaka huu dhidi ya Mauritius . Mechi ya mwisho katika
hatua hiyo itakuwa Julai 10 mwaka huu dhidi ya Namibia .
Kundi B lina timu za Kenya
(Harambee Stars), Botswana
(Zebras), Lesotho na Swaziland .
Hatua itakayofuata baada ya hapo ni ya mtoano (knockout) na kila kundi litatoa
timu moja tu.
Iwapo Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro
Premium Lager itafuzu kwa hatua itakayofuata itacheza Julai 13 mwaka huu na
Afrika Kusini (Bafana Bafana) ambayo pamoja na timu nyingine tano zimekwenda
moja kwa moja katika hatua ya mtoano.
Nyingine zilizokwenda moja kwa moja hatua ya
mtoano ni wenyeji Zambia , Angola , Zimbabwe ,
Msumbiji na Malawi
ambazo kwenye viwango vya ubora vya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu
(FIFA) ziko juu ya zile zilizoanzia hatua ya makundi.
Kwa mujibu wa ratiba hiyo, fainali ya michuano
ya Kombe la COSAFA itafanyika Julai 20 mwaka huu.
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa
Miguu Tanzania (TFF)
No comments:
Post a Comment